SIFA KUMI (10) ZA MSINGI KWA WAOMBAJI WA MIKOPO HESLB - EDUSPORTSTZ

Latest

SIFA KUMI (10) ZA MSINGI KWA WAOMBAJI WA MIKOPO HESLB


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUUJE, UTAOMBA MKOPO WA ELIMU YA JUU MWAKA HUU? 
1. Mwombaji awe Mtanzania.

 2. Mwombaji awe ameomba kudahiliwa na Chuo Kikuu au Taasisi ya Elimu ya Juu inayotambuliwa na Serikali.

3. Asiwe mwanafunzi wa masomo ya jioni (Part time Student).

4. Asiwe na udhamini/ufadhili/msaada wa kifedha kutoka katika vyanzo vingine.

5. Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa mtandao (OLAMS).

6. Awe amefaulu mitihani ya mwisho wa mwaka (wanaoendelea na masomo) na matokeo yake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo na chuo chake.

7. Awe amemaliza Kidato cha Sita au awe na sifa linganishi (kama Diploma n.k) ndani ya miaka mitatu (2015/2016 – 2017/2018).

 8. Awe na umri usiozidi miaka 30 wakati wa kufanya maombi.

 9. Waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja Waandamizi katika Makampuni binafsi yanayotambuliwa na Mamlaka za Mapato na Usajili hawatarajiwi kuomba;

10.Waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa umma au kisiasa ambao wanatajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma hawatarajiwi kuomba mikopo. Mwisho wa kuomba mkopo in Septemba 4, 2017 Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2017/18 unaopatikana kwenye tovuti: www.heslb.go.tz Imetolewa na: Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz