BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 8 August 2017

Real Madrid na Manchester United kushuka dimban leo

Washindi wa Ligi ya Europa Mancheter United watakutana na washindi wa ligi ya mabingwa Real Madrid katika Uefa Super Cup huko Skopje Macedonia.

United walianza na Meneja Jose Mourinho kwa kuwashinda Leicester katika mechi ya ngao wa jamii Agosti iliyopita.

Ikiwa Manchester United itaishinda Real Madrid itakuwa mara ya nne katika historia, watakuwa wameshinda vikombe vinne katika muda mfupi.

Manchester United wameshinda mara mbili dhidi ya Real Madrid kwenye mechi 10.

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Cristiano Ronaldo, ambaye amefunga mabao 16 kwenye mechi 10 zilizopita amejumuishwa kwenye kikosi cha Real pamoja na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 alipewa likizo baada ya kushiriki mechi za kombe la mabara, kabla ya kufika mbele ya mahakama nchini Uhispania kujibu mashtaka yanahusu kodi yake.

"Kumekuwa na mambo mengi ambayo yemekuwa yakiendelea, kelele nyingi zinazomzunguka lakini ametulia," Kocha wa Madrid Zinedine Zidane alisema.

"Kinachonifurahisha zaidi kumhusu ni kuwa kimwilim,yuko vile alikuwa wakati wa fainali ya ligi ya mabingwa ambayo ilichezwa miezi miwili iliyopita.

Muda wa mapumziko wa kupata vinywaji wakati wa mechi, utakuwepo ikiwa joto litaendela kushuhudiwa hadi leo Jumanne.

Joto hilo kwa jina 'Lucifer' limekumba eneo la kusini mwa Ulaya huku joyo huko Macedonia likipana hadi nyuzi joto 40.

No comments:

Post a Comment