OKWI AWEKA WAZI NIA YAKE KWA SIMBA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 26 August 2017

OKWI AWEKA WAZI NIA YAKE KWA SIMBA
Mshambulizi nyota wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda, amesema kuwa kuanzia leo katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani atapambana kuhakikisha anafunga na kuipa ushindi timu yake.
Okwi aliyesajiliwa na Simba kwa mara nyingine akitokea SC Villa ya Uganda, licha ya kucheza michezo sita hadi sasa ukiwemo wa Yanga, amefunga mabao mawili pekee.


Okwi amesema kutokana na kutofunga mabao mengi, atajitahidi kuanzia leo kwenye mchezo dhidi ya Ruvu afunge ili kuipa ushindi Simba.


"Sipo tayari kuiona timu yangu inakosa matokeo, hivyo nitapambana leo nifunge ili tupate ushindi ambao mashabiki wetu wanahitaji.

"Lakini ili niendelee kulilinda jina langu lisishuke basi nitahakikisha nafunga kila mchezo ulio mbele yangu kwa maana kikosi chetu ni kizuri na kuna watu wazuri na wenye uwezo mkubwa, hivyo ushindi kwetu ni lazima kwa kila mchezo," alisema Okwi.

No comments:

Post a Comment