NIYONZIMA:NITAKULA SAHANI MOJA NA YANGA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 26 August 2017

NIYONZIMA:NITAKULA SAHANI MOJA NA YANGA


Haruna Niyonzima.
KIUNGO wa Simba, Haruna Nyiyonzima, amekiri ugumu wa mechi yao ya leo Jumamosi dhidi ya
Ruvu Shooting, lakini anaamini timu nyingi ikiwemo Yanga zipo vizuri na wao watapambana nazo ili watwae ubingwa.

Simba inaanza Ligi Kuu Bara kwa kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa halafu kesho Jumapili Yanga itacheza na Lipuli FC ya Iringa uwanjani hapo katika muendelezo wa ligi hiyo.Niyonzima ambaye leo ataichezea Simba mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu tangu ajiunge nao akitokea Yanga, amesema mbali na timu zote kujiandaa vizuri, watapambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa.Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema kikosi chao kina mastaa wengi wanaoweza kuamua matokeo mazuri, lakini watatakiwa kupambana kwa kila hali katika kila mchezo ulio mbele yao ili wapate ushindi.“Kila timu ipo vizuri, Yanga wapo vizuri na wanautaka ubingwa, hivyo na sisi tumejipanga kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote japokuwa nyingi ni ngumu ikiwemo hii ya kesho (leo).“Hatuna njia rahisi ya kutwaa ubingwa bila kupambana kwa juhudi zote, sisi ni wazuri kila upande jambo ambalo naamini litazifanya timu pinzani kutukamia ili tusiweze kupata matokeo, ila tutapambana,” alisema Niyonzima raia wa Rwanda.A

No comments:

Post a Comment