MZEE KILOMONI KUTUNISHA KIFUA SIMBA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Sunday, 20 August 2017

MZEE KILOMONI KUTUNISHA KIFUA SIMBA
Mkutano mkuu wa Simba uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam iliamua kumuondoa Hamisi Kilomoni katika bodi ya wadhamini na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Mgoyi huku kaimu rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah akieleza Kilomoni kusimamishwa uanachama hadi atakapofuta kesi mahakamani na la asipofanya hivyo watamchukulia hatua zaidi.

Dar es Salaam. Achana na habari za kuondolewa katika bodi ya wadhamini wa Simba na kusimamishwa uanachama wa klabu hiyo huku akipewa sharti la kufuta kesi aliyofungua mahakamani, Mzee Hamis Kilomoni hana habari na masharti hayo na ameendelea kukomaa akisisitiza hafuti kesi.


Mkutano mkuu wa Simba uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam iliamua kumuondoa Hamisi Kilomoni katika bodi ya wadhamini na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Mgoyi huku kaimu rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah akieleza Kilomoni kusimamishwa uanachama hadi atakapofuta kesi mahakamani na la asipofanya hivyo watamchukulia hatua zaidi.


Kilomoni alisema hajafuta kesi kama ambavyo imekuwa ikivumishwa na hataifuta kesi hiyo hadi pale uongozi wa Simba utakapompelekea barua ya kusimamishwa uanachama na kuondolewa kwenye bodi ya wadhamini.


"Nangoje barua ya uamuzi huo, ninachojua mimi bado niko Simba kwa kuwa sijapewa barua rasmi hadi sasa (juzi jioni)," alisema Kilomoni bila kutaka kuzungumzia zaidi suala hilo.


"Siwezi kulizungumzia kwa kina sababu sina barua, nitakapoletewa barua rasmi ndipo nitakuwa katika nafasi ya kulizungumzia," alifafanua Kilomoni.


Kuhusu taarifa za yeye kufuta kesi mahakamani, Kilomoni alisema hajafuta na hawezi kufanya hivyo hivi sasa ingawa hakutaka kuzungumzia kama atakuwa tayari kufuta kesi endapo ataletewa barua hiyo.


"Narudia tena nikishapewa barua rasmi nitakuwa kwenye nafasi ya kuzungumza kila kitu, najua klabu yetu ina matatizo mengi, lakini yote tuyaache kwanza nisubiri barua yangu ya kusimamishwa kwanza," alisema Kilomoni.


Hata hivyo, Simba ambayo kesho Jumapili itakuwa na mkutano wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu yao mkutano utakaofanyika jijini Dar es Salaam, uenda ikalijadili kwa mara nyingine sakata la Kilomoni.


Kaimu rais wa Simba, Salim Abdallah alisema wanachama wa klabu hiyo wataamua suala la Kilomoni endapo hataridhia kufuta kesi aliyofungua mahakamani.