MAKONDA; SITODHUBUTU KUTOA KAULI YA SAMAHANI KWA CLOUDS NA WANAHABARI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 10 August 2017

MAKONDA; SITODHUBUTU KUTOA KAULI YA SAMAHANI KWA CLOUDS NA WANAHABARI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesisitiza kwamba kamwe hataomba radhi kufuatia sakata la kudaiwa kuvamia Clouds Media, akidai kwamba hakuwa amefanya kosa lolote na kwamba yeye na Ruge ni marafiki wa siku nyingi.

Makonda aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari, wakati wakieleza hatua zilizofikiwa katika usuluhishi wa mgogoro kati yake na Clouds Media chini ya Ruge Mutahaba, kufuatiwa kufungiwa kwake na vyombo vya habari kutochapisha au kutangaza habari zinazomhusu.Ruge ma Makonda, baada ya kuwa na bifu kwa muda mrefu, hivi karibuni walipatanishwa na mheshimiwa rais, John Pombe Magufuli alipokuwa kwenye mkutano mkoani tanga ambapo aliwaita wote wawili jukwaani na kuwataka wamalize tofauti yao.