Maamuzi ya Mahakama ya Kisutu kuhusu Mkutano wa Simba SC - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 12 August 2017

Maamuzi ya Mahakama ya Kisutu kuhusu Mkutano wa Simba SC

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu usiku wa jana iliyatupilia mbali maombi ya Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Simba walioomba kusitisha Mkutano Mkuu wa Jumapili Agosti 13, 2017.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema anakubaliana mapingamizi ya wajibu maombi kwamba wapo baadhi ya wajumbe wameanza kufika Dar es Salaam na kwamba Klabu hiyo imelipia ukumbi akiongeza kuwa ameona gharama isiwe kubwa na kwamba waleta maombi wanaweza kupeleka malalamiko yao katika mkutano huo.