KINACHOMFANYA NEYMER AONDOKE BARCELONA - EDUSPORTSTZ

Latest

KINACHOMFANYA NEYMER AONDOKE BARCELONA



Romario alishinda taji la mchezaji bora duniani 1994. Ikawa ni zamu ya Ronaldo kushinda 1996 na 1997 na tena 2002.


Romario alishinda 1994. Ikawa ni zamu ya Ronaldo kushinda 1996 na 1997 na tena 2002.

Rivaldo alichaguliwa 1999, Ronaldinho 2004 na 2005 huku kaka akichaguliwa 2007.

Katika kipindi cha miaka 13, wachezaji watano walishinda taji la mchezaji bora dunia katika miaka 8 tofauti hivyobasi kuweka mfano mwema miongoni mwa vipaji vya kizazi kipya.

Uchezaji wa Neymar utaonekana na yeye mwenyewe na raia wengine wa Brazil kama ambaye atakosa mafanikio makubwa iwapo hatashinda taji hilo.

Na iwapo unataka kujua ni kwa nini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anataka kuondoka Barcelona kuelekea PSG basi ni muhimu kuelewa kwamba atakumbukwa nyumbani Brazil.

Mbali na hilo kuna swala la kwa nini PSG inaweza kuwa hatua ambaye angepende kushinda taji ambalo limemkwepa.

Kama ufanisi wowote, kutoshinda pia ni mojawapo ya maswala yanayomkabili Neymar.

Kuna kushindwa kwake katika michuano ya dunia ya vijana wasiozidi miaka 17 nchini Nigeria 2009 wakati ambapo Brazil ilikuwa miongoni mwa timu nane zilizoshindwa kufaulu katika michuano ya kimakundi.

Safu ya mashambulizi inayoongozwa na Neymar, Coutinho haikufanikiwa kupata mabao wakati ilipohitajika kufanya hivyo.

Akishindwa kuonyesha umahiri wake, Neymar alitolewa nje wakati Brazil ilipokuwa nyuma 1-0 dhidi ya Mexico na Switzerland.

Alikuwa nyota chipukizi katika timu kubwa ya Santos katika ligi ya kwanza ya Brazil.

Funzo lilikuwa wazi: Soka ya kimataifa ilikuwa ngumu na alitarajiwa kuwa tayari kabla ya kuelekea Ulaya.

Chelsea ilidhani imempata wakati mmoja, lakini akakataa kuondoka Santos 2013.

Swala lengine ni kwamba Neymar alikuwa akimpenda sana Robinho aliyewahi kuichezea Santos.Neymar na Ribinho wakiichezea Barcelona

Wakati Robinho alipoelekea Real Madrid 2005 ilidhaniwa nchini Brazil kwamba mchezaji huyo atashinda taji hilo la mchezaji bora duniani.

Mchanganuzi mmoja, aliyekuwa wakati mmoja mshambuliaji wa Brazil Casagrande , alihisi kwamba Robinho angekuwa bora zaidi ya mchezaji mwengine yeyote isipokuwa Pele.

Historia inatuelezea mengine, na mchezo wa Robinho ulishindwa kufufuka baada ya kugundua kwamba Real Madrid walikuwa wakijiandaa kumtumia ili kumpata Cristiano Ronaldo -uamuzi ambao ulionekana kuwa mzuri.

Neymar baadaye alijua kwamba ili kuutawala ulimwengu katika soka angebidi aimarike hatua baada ya hatua hivyobasi akajiunga na Barcelona.

Timu ya Barcelona ambayo Neymar alijiunga nayo 2013 ilikuwa timu ya Lionel Messi.

Aliyekuwa winga wa Brazil Denilson kwa mfano alivunja rekodi ya dunia kama mchezaji aliyenunuliwa kwa kitita kikubwa miongo miwili iliopita lakini akalazimika kuichezea Real Betis.

Neymar hangekuwa na tatizo kama hilo.

Alifanikiwa kujiunga na klabu kubwa Ulaya chini ya kivuli cha Messi.

Lakini katika mpango huo wa hatua baada ya hatua , hangependa kuwa chini ya kivuli cha Messi kabisa.

Je, angeshinda vipi taji la mchezaji bora duniani licha ya kutokuwa mchezaji bora wa Barcelona?

Hivyobasi ilitarajiwa kuwa ni aidha Messi aondoke ama Neymar.

Na iwapo Messi ataondoka basi Neymar atachukua mahala pake .

Messi ametia kandarasi mkataba mpya. Amejiandaa kusalia kuwa mchezaji kiongozi wa klabu hiyo.Neymar baada ya kufunga bao dhidi ya Real Madrid

Huku rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu akiwa amesema kwamba Neymar hataondoka katika klabu hiyo.

Ripoti zimeendelea kuvuma kwamba PSG imempatia Neymar sababu ya kuondoka.

Msimu huu unakamilika na kombe la dunia, wakati ambapo Neymar yuko katika kilele cha mchezo wake.

Katika ligi ya Ufaransa ataweza kujinoa ili kuweza kuwa na gesi ya kutosha wakati wa michuano ya dunia nchini Urusi.

Ukweli ni kwamba Neymar kwa sasa anakabiliwa na mgogoro wa kibinafsi akivutwa pande tofauti na wito wa kutumia akili ama hisia

''Sitashangaa iwapo Neymar atasalia Barcelona ama iwapo ataelekea PSG'', kulingana na mshindi wa kombe la dunia 1970 TostaoNeymar, Messi na Suarez

"Neymar amejifunza mengi akiichezea Barcelona pamoja na Messi.

Hakuna tofauti kati ya raha anayopata upande mmoja baada ya kuichezea klabu kubwa duniani na urafiki alio nao na Messi na upande mwengine ari yake ya kutaka kuwa jina kubwa zaidi ya alivyo sasa.

"haiwezekani kutabiri ni chaguo lipi litakuwa zuri ama baya kwa Neymar.

Kitu kibaya ni kuwa na ndoto moja na baadaye kuchagua nyengine.

Babake, ajenti na mshauri wake wote wana mipango na maono, lakini hakuna anayejua raha ya kucheza pamoja na Messi na Luis Suarez katika klabu ya Barcelona


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz