KAPOMBE NAE ANENA KUHUSU MCHEZO WA WATANI ZAO WAJADI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 23 August 2017

KAPOMBE NAE ANENA KUHUSU MCHEZO WA WATANI ZAO WAJADI


Image result for Shomari KapombeBeki wa Simba, Shomary Kapombe, amesema kwa sasa anaendelea vizuri na majeraha ya nyonga yaliyokuwa yakimsumbua baada ya kupona na yupo tayari kuanza mapambano na kwamba leo Simba itashinda tu kwani wachezaji wenzake waliopo wana uwezo mkubwa.


Kapombe ambaye mara kwa mara amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo, hivi karibuni alijitonesha wakati anaitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilipocheza dhidi ya Rwanda kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki Michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan).


Kapombe amesema mchezo wa leo mbele ya watani zao, Yanga ana imani kubwa na kikosi kilichopo hivyo ana matarajio makubwa na ushindi.


“Kwa sasa naendelea vizuri kwani yale majeraha yangu yamepona na sisikii maumivu, muda wowote naweza kuungana na wenzangu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao, kuhusu mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii hakika nina imani na wachezaji wenzangu watatuwakilisha kwa ushindi.

“Sifurahii kukaa nje, nimekuwa nikipambana kuhakikisha napona haraka na kurejea uwanjani kuipambania timu yangu, kitu cha faraja ni kwamba kwa sasa naweza kufanya hivyo kutokana na kupona kwangu hivyo mchezo wa leo sina hofu kwani timu yangu ina uwezo wa kushinda bila mimi,” alisema Kapombe.

No comments:

Post a Comment