BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 2 August 2017

HATIMAYE NEYMER APATA TIMU MPYA


Nyota wa Barcelona Neymar amepewa ruhusa ya kuondoka Barcelona akitarajiwa kujiunga na PSG katika kitita cha rekodi ya pauni milioni 198.

Raia huyo wa Brazil amewaambia wachezaji wenzake wakati wa mazoezi siku ya Jumatano kwamba angependa kuondoka.

Alipewa ruhusa na meneja Ernesto Valvarde asifanye mazoezi na badala yake kushughulikia mpango wa uhamisho wake.

Mshambuliaji huyo ataruhusiwa kuondoka kwa gharama ya Yuro milioni 222, ambazo PSG iko tayari kulipa.

Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya kubainika kwamba Barca ilikuwa tayari kuruhusu uchunguzi wa Fifa iwapo PSG ingemsajili Neymar.

Katika mahojiano na gazeti la Mundo Deportivo, rais wa La Liga Javier Tebas alitishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa Ligue 1 iwapo soka ya Ulaya itashindwa kuchukua hatua.

Pia alisema kuwa rais wa PSG Nasser Al Khelafi alijulishwa kuhusu malengo ya mabingwa hao wa Uhispania.

Neymar alihamia Barcelona kutoka klabu ya Santos nchini Brazil 2013 kwa uhamisho wa pauni £46.6m na kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Uhispania 2016.

No comments:

Post a Comment