GARETH BARRY TIARI VITANI NA WEST BROM - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 17 August 2017

GARETH BARRY TIARI VITANI NA WEST BROM


Gareth Barry ni wa pili kwa kucheza mechi nyingi zaidi Ligi ya Premia

West Brom wamemnunua kiungo wa kati wa zamani wa England Gareth Barry kutoka Everton kwa bei ambayo haijafichuliwa.

Mchezaji huyo wa miaka 36 amecheza mechi 628 katika Ligi ya Premia katika misimu 21 akichezea Aston Villa, Manchester City na Everton.


Anahitaji kucheza mechi tano zaidi pekee kuvunja rekodi ya nyota wa Manchester United Ryan Giggs ya mechi 632.


Barry, ambaye alicheza misimu minne uwanjani Goodison, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja.


Meneja wa West Brom Tony Pulis amesema Barry ni mchezaji mzuri sana na anasubiri kwa hamu sana kufanya kazi naye.

Barry, ambaye amechezea timu ya taifa ya England mechi 53 ndiye mchezaji wa nne kununuliwa na West Brom kipindi cha sasa cha kuhama wachezaji baada ya Jay Rodriguez, Zhang Yuning na Ahmed Hegazi.


Pulis anatarajia Barry atajaza pengo lililoachwa na Darren Fletcher, aliyehamia Stoke.


West Brom walishinda mechi yao ya kwanza ya msimu kwa kulaza Bournemouth 1-0.


Lakini Pulis alionya kwamba wasiponunua wachezaji zaidi, watakuwa na wakati mgumu msimu huu.


"Tuna kikosi cha wachezaji 17 na wengi umri wao ni mkubwa," alisema Pulis.
Giggs alikuwa amecheza katika kila msimu Ligi ya Premia hadi alipostaafu Mei 2014. Alikuwa ameshinda mataji 13 ya ligi akiwa na Manchester United na kucheza mechi 632.


Barry, alicheza mechi yake ya kwanza msimu wa 1997-98 na amecheza zaidi ya mechi 30 kila msimu tangu wakati huo, isipokuwa katika msimu mmoja.


Miongoni mwa wachezaji ambao bado wanacheza, anayemkaribia ni Michael Carrick ambaye amecheza mechi 479.

No comments:

Post a Comment