EVERTON BEGA KWA BEGA NA MAN CITY - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Tuesday, 22 August 2017

EVERTON BEGA KWA BEGA NA MAN CITY


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWayne Rooney amefikisha jumla ya magoli 200 katika ligi kuu ya nchini England

Matajiri wa jiji la Manchester klabu ya Man city,imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Everton.

Everton almaarufu kama The Toffes, ndio walianza kuzifumania nyavu za Man City, kwa goli lilifungwa na mshambuliaji Wayne Rooney, Rooney amefikisha idadi ya magoli 200 katika michezo ya ligi kuu nchini England.

Katika dakika ya 82 Man City, walisawazisha goli hilo kupitia kwa winga Raheem Sterling aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Everton, Jordan Pickford.

Mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kubakia na wachezaji kumi baada ya beki wa City Kyle Walker, na kiungo wa Everton Morgan Schneiderlin, kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kila mmoja kuonyeshwa kadi mbili za njano.