BARCELONA YAMNASA MRITHI WA NEYMAR RAIA WA BRAZIRKlabu ya Barcelona imekamilisha usajili wa kiungo mbrazil, Paulinho kutoka Guangzhou Evergrande inayoshiriki ligi ya China kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 40
Nyota huyo wa zamani wa Tottenham mwenye umri wa miaka 29 atasaini mkataba wa miaka minne siku ya Alhamisi baada ya kukamilika kwa vipimo vya afya huku kukiwa na kipengere cha mkataba kinachosema kuwa endapo kama kuna timu itamtaka nyota huyo basi itatakiwa kulipa kiasi cha euro milioni ili kumsajili.
Paulinho ambaye atatambulishwa rasmi siku ya alhamisi kwenye dimba la Camp Nou anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na miamba hiyo ya Catalunya tangu walipomuuza Neymar kwenda PSG kwa euro milioni 222

Kiungo huyo mbrazili alishindwa kuonesha ubora kwenye ligi kuu ya Uingereza akiwa na Tottenham aliyojiunga nayo akitokea klabu ya Corinthians kabla ya kujiunga na Guangzhou Evergrande mwaka 2015.

Artikel Terkait