MICHEZO:HAJI MANARA ACHIWA HURU NA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF - EDUSPORTSTZ

Latest

MICHEZO:HAJI MANARA ACHIWA HURU NA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuachia huru Mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

Hayo yameweka wazi na Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu Abasi Tarimba katika mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa jana Jumatatu.

Manara alifungiwa na Shirikisho hilo baada ya kubainika utovu wa nidhamu wa kutoa matamshi yasiyo na staha kwa viongozi wa TFF pamoja na vyombo vya uongozi wa mchezo huo ambapo alihukumiwa muda wa miezi 12 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tisa adhabu iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF Wakili msomi Jerome.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz