BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 7 July 2017

Jezi atakayovaa Mbwana Samatta akiwa na KRC Genk 2017/18


Kutoka Ubelgiji anakocheza soka nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta, jana July 6 2017 zimeripotiwa taarifa za staa huyo kubadilishiwa namba ya jezi kutoka namba 77 na kupewa namba 10.

Samatta ambaye timu ya taifa huwa anatumia jezi namba 10 na akiwa na club yake ya KRC Genk anatumia jezi namba 77, kuanzia msimu wa 2017/18 atakuwa akivaa jezi namba 10 na sio namba 77.Sababu za Mbwama Samatta awali kuchagua kuvaa jezi namba 77 ni kwa sababu anapenda namba 7 kama anayotumia staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ambaye ni mchezaji anayemkubali ila Samatta anaamini ukienda katika timu mpya ni nadra kuikuta jezi namba 7 haina mtu.

No comments:

Post a Comment