BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 30 July 2017

CANNAVARO: HUKU MOROGORO TUPO FITI
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kambi yao iliyopo Morogoro ipo vizuri na wao wachezaji wapo fiti na amedai wanaisubiri mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ifike wafanye yao.

Mapema wiki hii, Yanga iliweka kambi Morogoro kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba itakayochezwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Wachezaji wa timu ya Yanga.

Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka Morogoro, Cannavaro amesema kambi yao ipo vizuri na inawajenga vizuri kuelekea mchezo wao na Simba na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.“Kambi yetu ni nzuri na tunaendelea vizuri, kila mchezaji yupo vizuri anajituma kuona anafanikiwa kufanya vizuri katika mazoezi kwani tunahitaji kuwa bora zaidi kwenye ligi na mechi nyingine tutakazocheza.“Mechi ya watani itakuwa nzuri na yenye upinzani mkubwa kwa pande zote mbili na mara nyingi huwa haina mwenyewe hivyo dakika tisini ndizo zitaamua nani atakuwa mshindi, kwa upande wetu tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda,” alisema Cannavaro.Cannavaro alisema usajili uliofanywa na uongozi wa timu yake ni mzuri na utaleta ushindani kwenye ligi kutokana na aina ya wachezaji waliosajiliwa.Wakati Yanga ikiwa kambini Morogoro, Simba yenyewe ipo jijini Johannesburg, Afrika Kusini kujiandaa na mechi hiyo pamoja na msimu ujao wa ligi kuu.

No comments:

Post a Comment