VIDEO: Magoli 8 aliyofunga Usengimana anayedaiwa kasajiliwa na Singida kwa zaidi ya Tsh Milioni 200 - EDUSPORTSTZ

Latest

VIDEO: Magoli 8 aliyofunga Usengimana anayedaiwa kasajiliwa na Singida kwa zaidi ya Tsh Milioni 200




Jina la Danny Usengima kwa soka la Rwanda sio geni lakini kwa Tanzania inawezekana ndio ukawa unalisika kwa sasa baada ya club ya Singida United ya Tanzania, kutangaza kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili akitokea club ya Polisi FC inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda.


Danny Usingimana ndio mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda kwa misimu miwili mfululizo na msimu uliyomalizika amefunga jumla ya magoli 19 na kuwa mfungaji bora, kuanzia msimu ujao utamuona akicheza Singida United ambao hawajaweka wazi dau walilomsajili.

Staa huyo anayeitumikia pia timu ya taifa ya Rwanda mtandao rwanda-foot.com wa Rwanda umeripoti kuwa staa huyo wa Rwanda, amesajiliwa kwa dola 100,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200.

Unaweza kutazama video ya magoli nane aliyowahi kufunga Danny Usengimana




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz