BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 24 June 2017

Baada ya kukalishwa benchi msimu mzima aibukia U21.
Winga wa timu ya taifa ya England ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 Demaria Gray amesema amefurahishwa na usiku wa manane wa Leicester baada ya yeye kufunga goli lake la kwanza baada ya msimu mzima kua benchi.

Demaria ambae msimu uliomalizika hakubahatika kuanza katika kikosi cha timu ya The foxes(Mbweha) alichokua akikitumikia na kukosa kuanza katika michezo miwili ya awali ya timu yake ya taifa, amepata bahati hiyo baada ya kuonyesha uwezo wake baada ya kuifungia timu yake ya taifa goli moja huku akitengeneza nafasi ya goli lingine katika ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Poland.

Akiongea na Dailystar.co.uk amesema "Nina hasira na ninataka kufanya jambo,Nilikalishwa benchi msimu mzima ,iliniathiri sana." Aliendelea kusema " licha ya hilo nilizidi kujipa tumaini juu ya mashindano haya.
"Nimeusahau msimu ulioisha nauanza msimu mpya nikiwa na Leicester lakini kwa sasa nahitaji kuwrka nguvu kwenye mashindano zaidi kwanza."Alisema Demaria.
Aliendelea kuongeza kwa kusema sikuanza katika michezo miwili iliyopita ila niliendelea kujipa moyo.


Demaria alijiunga na Leicester akitokea Birmingham kwa ada ya £ 3.7m mnamo January mwaka 2016

No comments:

Post a Comment