Type something and hit enter

On
Image result for simba

MASHABIKI wa Simba hakuna wanachokiwaza kwa sasa zaidi ya timu yao kutwaa ubingwa wa Kombe la FA, ili kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Simba inatarajia kucheza fainali ya michuano hiyo Mei 28, mwaka huu, kwa kukipiga na Mbao FC, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma.
Ili kunogesha ushiriki wao kimataifa, mashabiki hao tayari wameanza kuwaota nyota wapya wa kuboresha kikosi chao, wakiwataja straika Donald Ngoma, winga Simon Msuva na beki Juma Abdul kutoka Yanga.
Kupitia mitandao ya kijamii, mashabiki wa Simba wamekuwa wakianika kikosi kipya cha Simba msimu ujao ambacho wanaamini kikiwepo na wachezaji hao kitarudisha hadhi ya Simba kimataifa kama ilivyokuwa mwaka 2003.
Kikosi cha kwanza ambacho mashabiki hao wanakihitaji ni kama ifuatavyo: Langoni anaanzishwa kipa Daniel Agyei, Juma Abdul, Mohammed Hussein`Tshabalala` Jjuuko Murshid, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Saimon Msuva, Mzamiru Yassin, Laudity Mavugo, Donald Ngoma na Emmanuel Okwi.
Mbali na kuwataja wachezaji hao, lakini pia wamekuwa wakiutaka uongozi wa klabu hiyo kusajili wachezaji ambao watachukua nafasi zao, huku miongoni mwao akitajwa winga wa Mwadui FC, Hassan Kabunda.
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment