MSIBA: Dogo Mfaume wa ‘kazi ya dukani’ amefariki - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 17 May 2017

MSIBA: Dogo Mfaume wa ‘kazi ya dukani’ amefariki

Kama sikio lako huzitegea sana nyimbo za bongofleva basi na ‘kazi ya dukani’ inaweza kuwa moja ya zile unazozijua…. na ni ngoma ambayo ilifanywa na Msanii aitwae Dogo Mfaume ambaye leo tumepokea taarifa za kifo cha Mfaume kutoka Muhimbili Hospital.

Mmiliki wa Sobber House alikokua akisaidiwa ili kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya amesema ‘alikua afanyiwe upasuaji Ijumaa kutokana na uvimbe kwenye ubongo na alikua tayari ameshapangwa kwenye ratiba’

‘Afya yake ilikua nzuri kabisa na alikua ana mwaka mmoja toka ameacha utumiaji wa dawa za kulevya ‘unga’ na tulikua tumejiandaa kesho twende tukamtolee damu’

Akiongea huku analia Mmiliki huyo wa Sobber House ameendelea kueleza >>> ‘Afya yake ilikua nzuri kabisa na aliniambia dada mimi sitaki kuondoka kwako nataka unisimamie kila kitu na sitaki kurudi mtaani, mtaani hali mbaya na nikikaa kule nitarudi kutumia unga”

“Aliniambia naomba nisimamie tu mimi nakaa hapahapa…… masikini ya Mungu huu uvimbe eeeh Mungu jamani… amefariki na wameshamzungushia na kile kitambaa cha kijani‘

R.I.P Dogo Mfaume

No comments:

Post a Comment