MFUNGAJI BORA LIGI KUU TANZANIA BARA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 21 May 2017

MFUNGAJI BORA LIGI KUU TANZANIA BARA
Abdulrahaman Musa wa Ruvu Shooting ndiye shujaa katika msimu huu wa Ligi ya VPL uliohitimishwa May 20, 2017.
Abdulrahaman katika msimu huu wa Ligi amecheza dakika 2,700 katika michezo yote 30 iliyochezwa na kila timu pasipo kupumzika na kufanikiwa kufunga magoli 14 kati ya hayo, mawili yakiwa ya pinati.

Magoli aliyofunga Abdulrahaman ni dhidi ya Simba (1), mzunguko wa kwanza, Taifa, Yanga (1), mzunguko wa kwanza, Taifa, Ndanda Fc (1, penati), mzunguko wa kwanza, Mabatini, Mbao (1), mzunguko wa kwanza, Mabatini, JKT Ruvu (2), moja kila mchezo, nyumbani na ugenini, Majimaji (3), mzunguko wa pili, Mabatini, Mbeya City (1), mzunguko wa pili, Sokoine, Mbeya, African Lyon (1), mzunguko wa pili, Chamazi Complex, Mwadui (1, penati), mzunguko wa pili, Mwadui Complex, Shinyanga na Stand United (1), mzunguko wa pili, Kambarage Shinyanga.

No comments:

Post a Comment