Azam FC kumalizana na John Bocco - EDUSPORTSTZ

Latest

Azam FC kumalizana na John Bocco


Image result for john boko

Siku moja baada ya mitandao ya kijamii kuandika kuwa mshambuliaji wa Azam FC John Bocco amejiunga na Simba, taarifa ambazo bado hazina uhakika wowote, leo May 26 Azam FC  kuachana na John Bocco.

Azam FC leo kupitia kwa afisa habari wake Jafari Idd Maganga wameweka wazi kuwa John Raphael Bocco hatoendelea kuitumikia Azam FC kuanzia msimu ujao kutokana na mchezaji huyo kumaliza mkataba wake.

Jafari Idd kupitia SportExtra ya Clouds FM amethibitisha kuwa John Bocco sio mchezaji wao tena hivyo swali au ishu yoyote inayomuhusu John Bocco atafutwe mwenyewe


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz