Yanga wapewa mkopo wakate tiketi kurudi Bongo - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 17 April 2017

Yanga wapewa mkopo wakate tiketi kurudi Bongo

Wachezaji wa Yanga wanatarajia kuondoka leo usiku nchini Algeria kurejea nyumbani.
Sasa wanatarajia kuondoka na ndege ya Emirates badala ya Turkish Airways na imeelezwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limelazimika kutoa mkopo kwa klabu hiyo ili kuwakomboa.
Wachezaji saba na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa walichelewa ndege jijini Algeria na kulazimika kusubiri hadi Jumanne kesho ndiyo waondoke na kutua nchini kesho.
Mkwasa alisema wataomba msaada kwa MC Alger waliokwenda kucheza nao na kufungwa mabao 4-0 kwa kuwa hawakuwa na fedha za kutosha.
Lakini msaada huo wa TFF utawafanya warejee haraka nyumbani na si Jumatano tena kama ambavyo ilikuwa ikitarajiwa

No comments:

Post a Comment