BEKI WA KATI WA CHELSEA JOHN TERRY ATANGAZA KUG'OKA KLABUNI HUMO - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 18 April 2017

BEKI WA KATI WA CHELSEA JOHN TERRY ATANGAZA KUG'OKA KLABUNI HUMONahodha wa mda mrefu wa klabu ya Chelsea John Terry ametangaza rasimi kuondoka klabuni humo baada ya kutumika kwa mda mrefu katika klabu hiyo.

Terry mwenye umri wa miaka 36 kwa sasa, alijiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 15 akitokea katika klabu ya Westham ambazo hizi ni klabu za vijana (Youth career).

Terry alikaa na klabu hiyo ya Vijana ya ya Chelsea kuanzia 1995-1998 ambapo alijiunga na klabu ya Chelsea anayoitumika kwa sasa akiwa na umri wa miaka 17.

Hata hivyo mnamo mwaka 2000 Terry alitolewa na kwenda Nottingham forest kwa mkopo na baadae kurejea darajani hadi sasa.

Terry amekua na mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika klabu hiyo kwani aliiwezesha kutwaa makombe mbalimba ikiwemo ligi kuu England mara 4 ,FA Cup mara 4 ,Kombe la ligi(Capital one) mara tatu 3,na klabu bingwa Ulaya mara moja.

No comments:

Post a Comment