Tulieni, vyuma vinashuka muda si mrefu - Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Tulieni, vyuma vinashuka muda si mrefu - Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewashukuru wanachama, mashabiki wa wapenzi wa Yanga kwa imani waliyoonyesha kwake akiwa ametimiza mwaka mmoja katika nafasi hiyo


Arafat amewataka Wanayanga waendelee kuwa na imani na uongozi wao chini ya Rais Injinia Hersi Said kwani malengo yao ni kuleta mafanikio zaidi Jangwani


Akizungumzia usajili, Arafat amewataka Wananchi kuwa na amani kwani muda sio mrefu watatangaziwa wachezaji waliosajiliwa kuongeza nguvu kikosini


Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat ameandika ujumbe huu;


"Wiki kama hii mwaka Jana, wanachama wa Yanga walitumia haki yao ya kikatiba, waliniamini na kunichagua kuwa Makamu wa Rais klabu yetu pamoja na uongozi mzima wa Yanga. Julai 10, 2023 nimetimiza mwaka mmoja nikiwa Makamu wa Rais wa Yanga.


Natumia fursa hii kuwashukuru wanachama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kwa imani kubwa mliyonayo kwangu na uongozi mzima uliopo madarakani.


Msimu uliopita (2022/23) ulikuwa ni msimu wetu wa kwanza madarakani, tumefanikiwa kushinda mataji yote tuliyoshiriki kwenye mashindano ya nyumbani lakini kwa upande wa mashindano ya kimataifa tumefika Fainali ya Kombe la Shirikisho na kumaliza katika nafasi ya pili.


Wananchi naomba muendelee kuniamini pamoja na uongozi mzima wa Yanga chini ya Rais wetu Injinia Hersi Said ili tuendelee kuipeleka klabu yetu kwenye mafanikio zaidi.


Ile Ahadi yetu iliobakia kwa timu zetu nyengine sasa wakati wake ndio umefika na tunakuja kuendeleza furaha Zaid.


Msitishwe na Wazee wa "Recycle Bin" vyuma vinashuka muda sio mrefu na ni vyuma kweli kweli na Mshindo Mmoja"Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz