Moloko amwaga wino Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Moloko amwaga wino Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Yanga maisha yanaendelea licha ya kocha wao Nasreddine Nabi kuwakimbia na viongozi wao wamemalizana na winga wao mmoja ambaye ni kama amepewa mkataba wa kocha huyo aliyetimka.


Uongozi wa Yanga umempa mkataba mpya winga wao Jesus Moloko kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo baada ya ule wa miaka miwili kumalizika msimu huu uliokwisha.


Yanga imempa Moloko mkataba wa mwaka mmoja ambao ni sawa na ule alioutumikia Nabi kwa mara ya mwisho ambao ulimalizika pia mwisho wa msimu huu kisha akagoma kuongeza mwingine.


"Tumeona tumpe mkataba mpya ni winga ambaye ameonyesha kiwango bora hasa msimu huu, tutampa nafasi ya kumuangalia katika mwaka mwingine kama ataendeleza kasi yake," alisema bosi mmoja wa juu wa Yanga.


Moloko ambaye aliimarika zaidi msimu huu amesaini mkataba huo akishinda vita ya awali kupigiwa hesabu za kusitishiwa mkataba wakati akimaliza mwaka wa kwanza.


Moloko awali Yanga ilipiga hesabu za kumtoa kwa mkopo kumpeleka Singida Big Stars wakati walipoona kiwango bora cha winga Mbrazil Frederico Dario ambaye hata hivyo baadaye alitimka klabuni hapo akirejea kwao.


Baada ya hesabu hizo iolikuwa ni kama zimemshtua Moloko ambaye alirudisha makali yake na kuifanya Yanga kumvuta mezani na kumpa mkataba mpya na wakati wowote atatambulishwa kuwa ataendelea kubaki.


Moloko kwa hatua hiyo huenda akawapiga chenga mawinga wenzakeTuisila Kisinda na Bernard Morrison ambao sasa watasubiri hesabu za kocha wao mpya kujua kama wataendelea au kubakizwa ndani ya klabu hiyo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz