Mashabiki 12 wafa kwa vurugu uwanjani - EDUSPORTSTZ

Latest

Mashabiki 12 wafa kwa vurugu uwanjani

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Takriban watu 12 wameuawa katika vurugu zilizotokea ndani ya Uwanja wa El Salvador, ambapo mashabiki wa soka walikusanyika kutazama mechi kati ya FC Alianza na Club Deportivo FAS. Taarifa ya polisi nchini humo imeeleza.


“Tuna matokeo mabaya ya waathiriwa 12, tisa ambao wako hapa uwanjani na wengine watatu ambao tumearifiwa wako katika vituo tofauti vya hospitali,” Mkurugenzi wa Polisi wa Kitaifa (PNC) Mauricio Arriaza amewaambia waandishi wa habari leo.


Polisi wamesema ripoti za awali zinaonesha mashabiki waliojaribu kuingia uwanjani katika mji Mkuu wa San Salvador wa Amerika ya Kati kutazama mechi kati ya FC Alianza na Club Deportivo FAS.


“Kulikuwa na milango miwili tu iliyofunguliwa katika uwanja mzima,” shabiki mmoja aliambia La Prensa Grafica. “Watu waliokuwa nje walitaka kuingia kwa nguvu, na wote wakatuangukia.”Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz