Ally Kamwe amuomba radhi Kocha Mgunda - EDUSPORTSTZ

Latest

Ally Kamwe amuomba radhi Kocha Mgunda

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amemuomba radhi Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Ramadhani Mgunda baada kutoa kauli ya kumkashfu mbele ya mashabiki wa Yanga.


Akiwa katika viwanja vya Mbagala Zakhem, Kamwe alimfananisha Kocha Mgunda na andazi jambo ambalo limeibua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari wengi wakidai kuwa Kamwe amemdhihaki Mgunda ambaye kiumri ni sawa na baba yake mzazi.


"Kwa unyenyekevu mkubwa, nichukue fursa hii kumuomba radhi Kocha Juma Mgunda kwa kauli yangu niliyoitoa leo kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala, Jijini Dar es Salaam.


"Nikiri, haikuwa kauli ya kiungwana na isiyokuwa na heshima. Nafsi yangu inanisuta, Nimemkosea sana. Niwaombe msamaha na wote niliowakwaza kwa kauli yangu," amesema AllyKamwe.


Kwa upande wake, Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amesema; "Uungwana na ukomavu wa kiwango kikubwa sana. Hakuna Bin Adam aliye mkamilifu duniani. Pole coach Mgunda na naungana na Ali Kamwe kukutaka radhi coach," amesema Kamwe.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz