Chama Cha waamuzi EPL chawaomba Radhi Brighton - EDUSPORTSTZ

Latest

Chama Cha waamuzi EPL chawaomba Radhi Brighton

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kamati ya waamuzi wa England, PGMOL, imeiomba radhi klabu ya Brighton & Hove baada ya kunyimwa penati ya wazi dhidi ya Tottenham Hotspur hapo siku Jumamosi.


Matokeo yakiwa 1-1, Brighton & Hove walistahili kupata penati baada ya mchezaji wa Tottenham Hotspur, Pierre-Emile Hojbjerg, kumshika ndani ya eneo la hatari Kaoru Mitoma wa Brighton & Hove.


Lakini mwamuzi Stuart Attwell akapeta kuashiria mchezo uendelee bila kujiridhisha angalau hata kuangalia VAR licha ya wachezaji wa Brighton & Hove kumtaka mwamuzi huyo kufanya hivyo.


Kocha wa Brighton, Roberto De Zerbi, alioneshwa kukerwa na tukio hilo na kumfuata mwamuzi kuzungumza naye kwa hasira.


Sasa Mkuu wa kamati ya waamuzi, Howard Webb, amejitokeza hadharani kwa niaba ya kamati kuwaomba radhi Brighton.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz