Serikali:Saluni Ziwapime Wateja Joto la Mwili Kabla Hawajaingia Ndani - EDUSPORTSTZ

Latest

Serikali:Saluni Ziwapime Wateja Joto la Mwili Kabla Hawajaingia Ndani
Wamiliki wa Saluni na Vinyozi wanatakiwa kuwa na vifaa vya unawaji mikono nje ya saluni ambapo kila atakayeingia katika eneo hilo atahitajika kunawa mikono au kutumia vitakasa mikono

Hakikisha uwepo wa taulo za kutosha zilizofuliwa, kukauka na kupasiwa kulingana na wingi wa Wateja. Kila Mteja atumie taulo lake lililo safi na pale ambapo Wateja huvishwa joho la kufunika mwili, Mhudumu ahakikishe mteja amezungushiwa tissue shingoni kabla ya kumvika joho hilo
-
Hakikisha hakuna msongamano wa Watu na kwamba kila kiti kiwe katika umbali wa mita moja na kuendelea na pale inaposhindikana wateja wasubiri nje. Hakikisha uvaaji wa barakoa muda wote kwa Watoa Huduma na Wateja


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz