Mjane wa Rais Aliyeuawa Arejea Haiti - EDUSPORTSTZ

Latest

Mjane wa Rais Aliyeuawa Arejea Haiti
MJANE wa rais aliyeuawa Haiti, Jovenel Moise amerudi nyumbani baada ya kutibiwa majeraha aliyoyapata katika shambulio.

Waziri wa mawasiliano wa serikali Frantz Exantus kupitia mtandao wa twitter ameandika kwamba Martine Moise, alipokelewa katika uwanja wa ndege wa Port-au-Prince na waziri mkuu wa mpito Claude Joseph.

 

Martine alilazwa katika hospitali ya Miami huko Florida nchini Marekani kwa siku 10 baada ya kushambuliwa pamoja na mumewe nyumbani kwao ambapo rais huyo aliuawa kwa kupingwa risasi mnamo Julai 7.

 

Mazishi ya kiongozi huyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 23 huko Cap-Haitien, jiji la kihistoria, kaskazini mwa Haiti, ambalo limeathirika vibaya na machafuko tangu kuuwawa kwa Moise.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz