ALICHOANDIKA ZITTO KUHUSU BAMBARDIER BADA YA HOTUBA RAIS - EDUSPORTSTZ

Latest

ALICHOANDIKA ZITTO KUHUSU BAMBARDIER BADA YA HOTUBA RAIS



Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo amefunguka na kusema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya awamu ya tano imekopa dollar milioni 500 kutoka benki ya Uswiss na pesa hizo ndiyo zimetumika kulipa ndege za Tanzania.

Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya jamii na kusema kuwa riba za mkpo huo ni mkubwa sana na kudai watu wa chini wakiwepo wavuvi wa Migebuka kutoka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao.
"Serikali ya CCM ya awamu ya Tano imekopa $500m kutoka Benki ya Credit Suisse ya Uswiss Kwa riba kubwa Sana. Sehemu ya fedha hizo zimetumika kulipia ndege ambazo Serikali inanunua. Wavuvi wa Migebuka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao" alisema Zitto Kabwe

Rais Magufuli leo amesema kuwa uchumi wa nchi unazidi kukuwa na kudai serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina pesa za kutosha ndiyo maana imeweza kununua ndege mpya zaidi ya sita kwa mara moja na kudai watu ambao wanasema uchumi umeshuka wanaichonganisha serikali na wananchi.



 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz