Man United, Arsenal kupewa vigogo Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulay - EDUSPORTSTZ

Latest

Man United, Arsenal kupewa vigogo Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulay

 Man United, Arsenal kupewa vigogo Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mambo ni moto. Manchester United na Arsenal huenda zikapangwa kwenye makundi magumu zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo droo ya upangaji wa hatua hiyo ya makundi utafanyika leo Alhamisi Monaco, Ufaransa.


Utaratibu wa upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya unakuwa na vyungu vinne (Pot), ambapo zinawekwa timu na kuchaguliwa mojamoja na kupata kundi lenye timu nne. Kwa ujumla wake timu zipo 32, hivyo zitaunda jumla ya makundi nane.


Arsenal na Man United zote zimepangwa kwenye Pot 2, hivyo zitakuwa na kibarua cha kumenyana na mwamba yeyote aliyewekwa kwenye Pot 1 isipokuwa Man City tu ambayo wanacheza kwenye ligi moja, Ligi Kuu England na hatua hii ya makundi timu za ligi moja haziruhusiwi kukutana.


Hali ilivyo, kwenye Pot 1, kutakuwa na timu mabingwa wa ligi za ndani pamoja na bingwa wa Europa League kwa msimu uliopita, hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2023-24, chungu hicho kitakuwa na timu za Manchester City, Sevilla, Bayern Munich, PSG, Barcelona, Napoli, Benfica na Feyenoord.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz