Matchday: Azam fc vs Simba Itazame LIVE hapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Matchday: Azam fc vs Simba Itazame LIVE hapa


 Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wako mkoani Mtwara ambapo jioni ya leo watashuka uwanja wa Nangwanda Sijaona kuikabili Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)


Mechi muhimu kwa Simba kuisaka fainali katika michuano pekee ambayo inaweza kuipa Simba taji msimu huu


Hautakuwa mchezo mwepesi kwani ni derby inayozikutanisha timu ambazo zina nafasi sawa katika kuhitimisha msimu huu


Kama ilivyo kwa Simba, Azam Fc wamefanya uwekezaji mkubwa wa kikosi chao hata hivyo uwekezaji huo haukuwapa mafanikio waliyotarajia


Matumaini pakee waliyonayo ni kutwaa taji la FA, kwao hii inaweza kuwa mechi kubwa zaidi msimu huu


Kwa misimu ya karibuni Azam Fc wamekuwa wagumu kila wanapokutana na Simba. Katika mechi mbili za Ligi Kuu, Azam Fc walishinda mchezo mmoja na kulazimisha sare katika mchezo mwingine


Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika michuano ya FA, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ukiwa ni mchezo wa nusu fainali mwaka 2021


Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira aliweka nguvu kubwa katika mchezo huu, akiwapa mapumziko nyota wake muhimu katika mchezo wa ligi kuu uliopita dhidi ya Namungo


Ni mazingira hayo yanayoufanya mchezo huu kuwa muhimu kwa Robertinho na benchi lake la ufundi, kwani kama matokeo yatakuwa tofauti na ushindi, watatishwa mzigo wa lawama kwa maamuzi waliyofanya kwenye mchezo dhidi ya Namungo


Sare dhidi ya Namungo Fc ni kama iliiondoa Simba kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu na sasa matumaini yamebaki kwenye FA


Wanasimba hawawezi kujivunia chochote msimu huu kama timu yao haitatwaa taji la FAMechi itakuwa LIVE kwenye app yetu bofya hapa kuidownload ili usipitwe na mechi hii na nyingine nyingiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz