MASTAA HAWA YANGA NI DABI YAO YA KWANZA - EDUSPORTSTZ

Latest

MASTAA HAWA YANGA NI DABI YAO YA KWANZA

AGOSTI 13 Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga v Simba.

Ni saa 1:00 usiku mchezo huo unatarajiwa huku kila timu ikiwea wazi kwamba inahitaji kupata ushindi.

Kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kuna mastaa wapya ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza kucheza mchezo wa Kariakoo Dabi kwa msimu wa 2022/23.

Miongoni mwao ni Gael Bigirimana ambaye  amesajiliwa kutoka Glentoran FC yeye ni kiungo ambapo anacheza nafasi ile inayochezwa na Khalid Aucho na Zawad Mauya amba hawa wapo tangu msimu uliopita.

Joyce Lomalisa kutoka GD Sagrada Esperanca huyu ni beki wa pembeni ambapo anacheza David Bryson anachukua mikoba ya Yassin Mustapha ambaye amesepa ndani ya Yanga.

Azizi KI kutoka ASEC Mimosas huyu ni kiungo mshambuliaji ambaye anakuja kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji.

Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chiefs anakuja kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji akishirikiana na Fiston Mayele.

The post MASTAA HAWA YANGA NI DABI YAO YA KWANZA appeared first on Saleh Jembe.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz