Msanii Joel Lwaga Ateswa na Mipaka iliyopo Kazi ya Bongo Flava na Waimbaji wa Injili - EDUSPORTSTZ

Latest

Msanii Joel Lwaga Ateswa na Mipaka iliyopo Kazi ya Bongo Flava na Waimbaji wa Injili




Muimbaji wa nyimbo za injili nchini, @joellwaga amedai ifike mahali kusiwe na mipaka kati ya muziki wa gospel na miziki mingine. Akitolea mfano nchi ya Ghana, Lwaga amedai Ghana hakuna mipaka kwenye muziki kama huku bongo,Kule hawana tuzo za Gospel bali wana tuzo za aina moja (za jumla) na huko ndani utawakuta wanamuziki wa aina yoyote ile. Kwahiyo kama ni muimbaji bora wa mwaka wa kiume,anaweza kuwa mtu wa Gospel au muziki wa kidunia.

Lwaga ambaye ameachia EP yake inayoitwa "TRUST", Amedai imefika mahali kibongo bongo ukiimba namna fulani hivi unaanza kunyooshewa vidole kitu ambacho amejitolea kukitokomeza.

Pia Lwaga amebainisha kufungua label ya Muziki wa Gospel itayoitwa HEAVEN CULTURE ENT kitu ambacho hakijawahi fanyika kabla nchini kuwapo kwa Label ya Muziki wa Injili na amedai hana tatizo kufanya Colabo na mtu wa Bongo Flava ilimradi maudhui yasiwe kinyume na imani yake.

Lwaga anadai endapo matabaka ya huyu anaimba muziki ule, huyu muziki huu yatakwisha basi hata wasanii wa Gospel wataanza kupata endorsement kama wasanii wengine. Lwaga ametilia mkazo kuwa hawezi kuwa balozi wa Bia (kilevi) labda Grand Malt.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz