Kocha.. Nabi agongewa 'misumari' Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha.. Nabi agongewa 'misumari' YangaNabi agongewa 'misumari' Yanga

KLABU ya Yanga ni kama imemgongelea 'misumari' Kocha Mkuu wao, Nasreddine Nabi, ya kuendelea kuwa imara katika kazi yake ya kukiimarisha kikosi chao baada ya kueleza bado ina imani kubwa na Mtunisia huyo huku ikikanusha vikali taarifa za kutaka kumtimua.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli, amesema kocha Nabi yupo mazoezini kama kawaida, na hakuna kitu kama hicho ambacho kinasambaa kwenye mitandao ya kijamii na huenda lengo ni kuwaondoa kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya Rivers United nchini Nigeria.

"Siwezi kuongelea tetesi ambazo zinakwenda kututoa kwenye mchezo wetu wa marudiano. Kama ingekuwa ni kweli basi tungekuwa tumeweka kwenye mitandao yetu rasmi ya kijamii. Mimi nipo, Haji Manara yupo, tungekuwa tumeshaliongelea, lakini kwa sababu halipo, hatuwezi kuliongelea," alisema Bumbuli.

Alisema Yanga imepoteza mechi mmoja tu, lakini haijapoteza mashindano, hivyo hawaamini kama kuna jambo baya lolote ambalo limefanyika la kuweza kumpa mechi mbili au kumwondoa.

"Kwa maana hiyo, kocha Nabi bado yupo yupo sana. Huwezi kumpima kocha kwa mechi moja, labda mechi tatu mpaka nne, ndiyo mnaweza kusema kuwa mbona kama tunapotea kwenye malengo yetu. Nawataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuzipuuza tetesi hizo kwa sababu ndizo zina lengo la kutuondoa kuangalia zaidi mchezo wetu wa marudiano," alisema.

Jumapili iliyopita Yanga ilichapwa bao 1-0 kwenye mechi ya hatua ya awali, Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Baada ya mechi hiyo, juzi zilizuka tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa viongozi wa klabu hiyo wamempa kocha huyo mechi mbili anazotakiwa kushinda, vinginevyo atatimuliwa, huku Mwinyi Zahera akitajwa kutaka kurithi mikoba hiyo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz