Mo Awapa Luis, Chama Sh 350Mil Waifunge Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Mo Awapa Luis, Chama Sh 350Mil Waifunge Yanga

KATIKA kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imeahidi kuwapa wachezaji akina Luis Miquissone na Clatous Chama Sh 350Mil kama itawafunga watani wao Yanga.Timu hizo zimepanga kuvaana kesho Jumamosi katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara utakaopigwa saa kumi na moja kamili kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kupata matokeo yoyote ya ushindi ili watangazwe mabingwa wa ligi kutokana na idadi ya pointi ambazo wamewaacha watani wao Yanga.Mmoja wa mabosi wa Simba ameliambia Championi Ijumaa kuwa, fedha hizo watapewa wachezaji hao kama bonasi kama wataifunga Yanga katika kuongeza morali ili kuhakikisha wanapata ushindi.

Bosi huyo alisema kuwa bonasi hiyo watapatiwa wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mfaransa Didier Gomes mara baada ya mchezo huo kumalizika.

Aliongeza kuwa mara baada ya wachezaji hao kutangaziwa bonasi hiyo, morali ya wachezaji imeongezeka kwa kiasi kikubwa kuelekea pambano hilo.

“Ili kunogesha shangwe za ubingwa wa ligi ni lazima mchezo huu wa dabi tuwafunge watani wetu wa jadi, Yanga, hiyo ndiyo sababu ya wachezaji kutangaziwa bonasi hiyo.

“Uongozi wetu umekuwa na kawaida ya kuwapa bonasi wachezaji katika kila mchezo wa dabi, lakini hii ya msimu huu imeonekana kuongezeka.“Hiyo ni kuhakikisha morali ya wachezaji inaongezeka kwa kiasi kikubwa watakapokuwa uwanjani katika kuhakikisha timu inapata ushindi utakaotupa ubingwa wa msimu huu,” alisema bosi huyo.

Simba kwa kupitia Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ hivi karibuni alisema: “Kila mchezo tunaocheza kunakuwa na bonasi ambayo inategemea na umuhimu wa mchezo husika katika kuongeza morali ya wachezaji ili tupate ushindi.”

STORI NA WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz