£135.5m KUMSAJILI DEMBELE BARCELONA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 26 August 2017

£135.5m KUMSAJILI DEMBELE BARCELONA

Barcelona yakubali kumsajili Dembele kwa £135.5m kutoka Dortmund

Barcelona Imekubali kandarasi ya kumsajili mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Ousmane Dembele
kwa kitita kinachotazamiwa kupanda hadi Yuro milioni 147 na kumfanya kuwa mchezaji wa pili aliyeghali katika historia ya soka.

Barca watalipa Yuro milioni 105 kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 ambaye amekubali kandarasi ya miaka mitano na atafanyiwa ukaguzi wa matibabu siku ya Jumatatu.

Mkataba huo umepitwa na ule wa Neymar wa uhamisho wa Pauni milioni 200 kwa klabu ya PSG.

Dembele hajaichezea Dortmund tangu mechi ya kombe la Supercup mnamo tarehe 5 mwezi Agosti.

Timu hiyo ya Ujerumani ilikataa ombi kutoka kwa Barcelona kumununua mchezaji huyo mnamo mwezi Agosti, wakati ambapo mchezaji huyo alikuwa amepigwa marufuku kwa kukosa mazoezi.

Dortmund imesema kuwa ilikataa ombi la Barcelona kwa kuwa halikuandamana na thamani ya mchezaji huyo pamoja na hali ya kichumi ya sasa.

No comments:

Post a Comment