BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label love. Show all posts
Showing posts with label love. Show all posts

Friday, 25 May 2018

25 May

HAYA NDIYO MAMBO 7 YANAYOWAUMIZA WANAUME KATIKA MAHUSIANO


mwanaume

MAMBO 7 YANAYOWAUMIZA WANAUME KATIKA MAHUSIANO

Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa.Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake.Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye

kukimbiwa.Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama.

Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubwa.

Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wanawake ili kuweza kujua nini cha kufanya kuhakikisha unamweka mwanaume karibu, asikuache.1. Chokochoko/Maneno Maneno

Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. Kutoridhika

Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.

Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.

Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.

3. Kulinganisha

Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’

Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.

Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.

4. Kuwa Tegemezi

Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.

Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.

5. Kutokuwa Muelewa

Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.


Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. Kujigamba/Maringo

Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.

7. Kuwa bize sana

Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Tuesday, 22 May 2018

22 May

Njia 10 za Kupata Mchumba Bora

Wachumba wakivalishana pete
Njia 10  za Kupata Mchumba Bora

wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake.ya mtu na kumhusisha na uhuni.

Monday, 7 May 2018

07 May

FAIDA 16 ZA KUFANYA MAPENZI SALAMA KIAFYA

Image result for ADVANTAGES OF SEX
Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.

1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo: Wanawake ambao hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.
2. Huongeza ukakamavu wa mifupa: Wanawake waliokoma kupata hedhi (menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kamaosteoporosis.

3.Hupunguza msongo wa mawazo: Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, musclerelaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.
4. Hupunguza maumivu: Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom).
5.upunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume: Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.


6.uongeza uwezo wa kunusa: Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo (brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu (brain olfactory bulb).

7.upunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema: Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi.

8.uongeza kinga ya mwili: Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina yaimmunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.
9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke: Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa.

10.udhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida: Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa.


11.tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini: Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.


12.Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke (vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection ).

13.Hufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini: Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.


13.Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako: Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.


14usaidia kuishi kwa muda mrefu: Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele. DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.
15. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.


17.uongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba: Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne. chanzo.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Thursday, 26 April 2018

26 April

Wasichana Wazuri Duniani | Nchi Zenye Wasichana Wazuri Duniani

Wasicha Wazuri Duniani

Moja ya wasichana wazuri duniani

Tunaona quotes nyingi zikisema kuwa uzuri uko ndani ya mtu, ni katika macho ya mtu kuangalia uzuri. ni kweli katika nafsi na kadhalika. Hata hivyo tunasisitiza kuwa nzuri ni mambo ambayo yanaonekana na yanayovutia macho. .
Hapa kuna orodha ya nchi kumi za juu na wanawake waliovutia sana. Nchi hizi zinasemekana kuwa na wanawake wazuri, wenye kuvutia na wenye kupendeza duniani. Hebu tuangalie:


Orodha ya Wasicha Wazuri Duniani

Liza Soberano - Ufilipino Uzuri .

10. Philippines

Watu wa Filipino wanajulikana kwa mtazamo wao mzuri na uzuri lakini kuna upande mwingine wa nchi hii. Ina mafanikio zaidi katika "Vipindi vya Urembo Bora Vya Kimataifa vya Kimataifa". 

Helen Flanagan - Mwanamke mzuri sana wa Uingereza.


9. Uingereza


Wanawake wa Uingereza wa leo ni mchanganyiko wa tamaduni tofauti ambazo ni kwa nini huja katika tani mbalimbali za ngozi na inaonekana. Wao ni wenye elimu, wenye busara na juu ya yote - nzuri. 

Eugenie Bouchard - Mchezaji Bora zaidi wa tenisi wa Canada .

8. Marekani / Canada


Wanawake wa Amerika ni furaha , huru na wanajua jinsi ya kujitunza wenyewe. Nje ya barabara ya Miami, NY na Los Angeles utaona wanawake wengi mzuri ambao wanajua kujitunza wenyewe kwa sababu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Tutachukua wanawake wa Canada na Amerika kwa kiwango sawa. Angalia wanawake kumi wenye moto zaidi zaidi nchini Canada .


Doutzen Kroes - Mwanamke Mzuri zaidi wa Kiholanzi .
7. Uholanzi (Wanawake wa Kiholanzi)Kwa urefu wa urefu wa 5'7 "na nywele za blonde, mwanamke Kiholanzi anastahili kuwa katika nafasi ya 7 katika orodha ya nchi zilizo na wanawake waliovutia zaidi ulimwenguni. Angalia orodha ya Maeneo Ya Juu 10 na Wasichana Wenye Nzuri .

Mfano Mzuri Mzuri wa Kiitaliano Cristina Chiabotto.

6. Italia

Unaposema juu ya uzuri wa classy, ​​unazungumzia wanawake wa Italia walio sasa kwa mtindo, mtindo na babies. 

Norelys Rodriguez - Uzuri wa Venezuela.

Venezuela


Wanawake kutoka nchi hii wana taji nyingi kutoka mashindano ya uzuri wa kimataifa na miili yao midogo, ndogo hufanya hivyo kwa wapiganaji wa juu kila mwaka.

4. Uturuki

Meryem Uzerli - Mwanamke wa Kituruki wa Sexiest.


Uturuki hufanya juu ya orodha yetu juu ya wanawake nzuri na kwa nini haipaswi hivyo? Wao ni photogenic na takwimu nzuri na kujifanya karibu na ukuu ambao unaweza tu kuhusishwa na wafalme na vichwa vya historia ya Kituruki. Ikiwa una shaka, fuata sabuni na vipindi vya Kituruki kwenye TV!

Mfano wa Kirusi Mzuri zaidi Irina Shayk

3. Urusi

.

Je, umeona Mwanasheria Mkuu wa Urusi ? Hiyo inapaswa kukupa wazo la uzuri nchini. Wanawake wa Kirusi wana mchanganyiko wa sifa za magharibi na mashariki kwa namna ya cheekbones ya juu, miili pana na mirefu yenye nywele.  

Mwanamke mzuri Kiukreni Ani Lorak.
2. Ukraine


Wakati Ukraine na Urusi ni sawa, tunaona kuwa wanawake wa Ukraine wanajishughulisha zaidi kuliko wale wa Urusi. (Kura yetu kubwa bado ni kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ingawa!) 

Adriana Lima - Wanawake Wazuri zaidi wa Brazili.

1. Brazil


Wanawake wa Brazil wanajulikana kwa maslahi yao katika kijamii na mila. Wanajua jinsi ya kujitegemea, wanafanya jukumu kubwa katika sherehe ambazo huingia nchini kila mwaka. Nchi ina wanawake bora zaidi duniani.

Nchi zenye wasichana Wazuri Duniani

Brazil
Ukrain
Urusi
Uturuki
Venezuela
Italia
Uholanzi
USA / Canada
Uingereza
Philippines


like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika

For Booking>>>
CALL>>>
Voda: +255757441463
JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI

Thursday, 19 April 2018

19 April

SABABU ZINAZOPELEKEA KUWEPO KWA MICHEPUKO KATIKA MAHUSIANOImage result for lovers
Niliwahi kusema ya kwamba ya kwamba “mchepuko ni dili feki” wengi wakabishana sana, na leo naomba kurudia kusema ya kwamba mchepuko ni dili feki kwa sababu michepuko ndio chanzo cha mifarakano ya ndoa zilizo nyingi ulimwenguni kote hii ni kwa mujibu wa utafiti usio rasmi lakini ndio ukweli wenyewe. Na miongoni mwa sababu inayopelekea kutokea kwa michepuko ni:

Saturday, 31 March 2018

31 March

Vyakula Vinavyoongeza Nguvu Za Kiume Mwilini


Vyakula Vinavyoongeza Nguvu Za Kiume Mwilini
Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. 
Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.


Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.


Sababu za kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.


1. Blueberry

Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume.


Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.


3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.


Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.


4. Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.


5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.


6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.


Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.


Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.


Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.

NINI MAONI YAKO? ACHA UJUMBE WAKO HAPA CHINI!!!

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

Friday, 23 March 2018

23 March

MAMBO MAKUU 3 YALETAYO FURAHA KATIKA MAHUSIANO


Uhusiano maridhawa katika ndoa ni kitu kinachohitaji kujituma kwa bidii kubwa. Ni kitu kinachohitaji subira, uelewa na upendo kwa pande zote mbili.

Wakati unapenda kumfanya mwenzio kuwa mwenye furaha, kuna mambo kadhaa unayoweza kuyafanya kuhakikisha nawe unapata furaha. Ukweli kama hutofanya mambo haya matano, hutokuwa na zana sahihi zinazokupa furaha katika maisha ya ndoa yako:

1. Kumuamini.

Imani ni ufunguo wa furaha katika maisha ya ndoa. Usipomuamini mwenza wako utaendelea kukosa utulivu na kuwaza kuwa yuko wapi, yuko na nani au anafanya nini. Stress na mashaka utakayoyapata kutokana na wasiwasi na hisia za kuhisi kile anachofanya vitakuondolea furaha yako.

Ili uwe na furaha unatakiwa kuwa na imani, kumuamini. Imani inaweza kuchukua muda mrefu kuijenga, lakini ni kitu nyeti sana. Hakikisha unamweleza mwenzako wasiwasi wako pindi jambo fulani linapokuwa haliko sawa. Inaweza ikawa ni kutoelewa tu, lakini ukiiruhusu shaka ishike hatamu, inaweza kugeuka kuwa tatizo kubwa zaidi. Usiiruhusu shaka itawale maisha yako. Usiiruhusu shaka ndio iongoze maisha yako. Jiamini na umuamini, hiyo ni dawa kiboko.

2. Kumpa nafasi.

Kama unataka kuwa na furaha na mumeo hakikisha unampa nafasi, usimbane. Muache ajumuike na marafiki zake au kushiriki mambo ya maana anayoyapenda. Humfanya apate fursa ya kuwa mbali nawe kwa muda fulani na kuongeza nishati mpya ndani ya moyo na akili yake.

Sio tu kwamba ataku-miss, bali pia itakupa fursa ya kuwa mbali naye. Mkitumia muda wote wa 24/7 kuwa pamoja haliwezi kuwa jambo zuri, na halitokuwa na afya kwenye uhusiano wa ndoa yenu. Anaweza kuwa na hisia za kudumaa au kuhisi kuwa hawezi kufanya vitu anavyopenda kuvifanya. Mnapopata fursa ya kuwa mbalimbali kwa saa kadhaa inawapa fursa ya kuungana tena baadae mkiwa na nguvu mpya.

3. Kutenga muda wa kukaa pamoja.

Wakati fulani tunashughulishwa mno na shughuli za maisha na utafutaji kiasi kwamba hatutengi muda kwa ajili ya wenza wetu. Ili kuwa na furaha ni muhimu kutenga muda maalum kwa ajili yake tu, hata kama ni dakika chache. Pia wekeni muda maalum kila wiki kwa ajili ya kunong'onezana ambapo hakuna watoto, hakuna marafiki au kitu kingine chochote, ni nyinyi wawili tu. Kumbushieni mahabba yenu na ladha ya muunganiko wenu.Pia ni jambo zuri kutenga dakika kadhaa kila siku kwa ajili ya kuwasiliana. Mnaweza kutumia muda huo kujadili siku yenu inavyoendelea au kuchombezana. Kuwa na utaratibu wa kutenga muda maalum wa kuwasiliana au kuwa pamoja utaupa nguvu uhusiano wenu na kukufanya kuwa mwenye furaha.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Monday, 12 March 2018

12 March

NJIA ZA KISAYANSI ZITAKAZOKUPELEKEA KUPATA MTOTO WA KIUME


Uzazi wa mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa mpango ila hata kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango.

Watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na kutengana kwa sababu hizi.

Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.

Leo ntamaliza kitendawili hiki kwa kutoa njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi…

Kitaalamu mbegu zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye mfuko wa uzazi lakini hufa haraka. lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke, hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiumeXY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..

Zifuatazo ni njia hizo tano kali…

1. Hakikisha unashiriki tendo la ndoa siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}

Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike na kutengeneza mtoto{fertilization}hii ni siku ya 14 KABLA YA KUONA DAMU YA MWEZI UNAOFUATA SIO BAADA YA KUONA SIKU ZAKO..

Kama wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
Pima joto lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila asubuhi , siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..

Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..

2. Wewe mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako..{sperm count}

Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake aanze ovulation.

Njia zingine za kuongeza mbegu ni weka korodani kwenye hali ya ubaridi:
kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na kuwekalaptop kwenye mapaja acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi.. matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.


3. Tumia style za ngono ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa{deep penetration}

Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume{XY} kufika haraka na kufanya fertilization na upande mwingine, muingiliano mdogo{shallow penetration}husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike.{XX}.


4. Hakikisha mwanamke anafika kileleni:

Mwanamke anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.


5. Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya ovulation;

Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya ovulation..EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Friday, 9 March 2018

09 March

SAYANSI ILIYOFICHUKA JINSI MTU ANAVYOANZA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

Image result for LOVE
Ishara ya upendo kwa wapendanao
Unapoingia katika mapenzi na mtu ubongo wako unatengeneza mchanganyiko wa kemikali na kuziachia mwilini. Kemikali hizi ni pamoja na Oxytocin, Phenylethylamine na Dopamine. Kemikali hizi huongeza mapingo ya moyo na kusisimua mwili. Na hali hii ndiyo tuyoita mapenzi au mahaba.
Hali hii ni sawa kabisa na ile ambayo watumiaji wa madawa ya kulevya wanaipata.

Kama walevi wa madawa,mtu ambaye ameingia katika mapenzi anaanza kuona vitu tofauti ni uhalisia. Vitu vinaonekana ni vizuri sana na ubaya unajificha kabisa. Unaona vile vitu vizuri tu ambavyo vinakufanya ujisikie vizuri na kupuuza vyote ambavyo vinakufanya ujisikie vibaya.

Ulevi huu unakufanya uone vile vitu ambavyo wewe na mpenzi wako mnafanana na kutupilia mbali vile vyote mnavyotofautiana na vibaya.
Unakufanya pia useme na kufanya vile ambavyo vinampendeza na kumfurahisha mpenzi wako pekee.

Hali hii itaendelea mpaka kilevi kikiisha nguvu na huweza kuchukua muda wa miezi 2 hadi miaka 2. Katika hatua hii, ubongo wako unaaacha kuzalisha kemikali hizi za mapenzi na unajikuta unashangaa ilikuwaje umekuwa na mtu huyo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Saturday, 17 February 2018

Monday, 12 February 2018

Thursday, 8 February 2018

Sunday, 4 February 2018

Friday, 2 February 2018

02 February

MBINU ZITAKAZO KUFANYA KUISHI NA MPENZI ANAYEPENDA PESA KAMA MFUKOImage result for women money

HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana.
Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao
wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha!

Thursday, 1 February 2018

01 February

MAGONJWA UNAYOTAKIWA KUYAPIMA NA KUYAJUA KABLA YA KUFUNGA NDOANDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.