EDUSPORTSTZ : education

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Showing posts with label education. Show all posts
Showing posts with label education. Show all posts

Tuesday, 15 October 2019

15 October

MATOKEO DARASA LA SABA 2019-NECTA PSLE Results 2019

NECTA PSLE Results 2019-MATOKEO DARASA LA SABA 2019

MATOKEO DARASA LA SABA 2019
MATOKEO DARASA LA SABA 2019


The results of the seventh class 2019 have been announced. NECTA has reported an increase of 3.78 percent. Graduates make up 81.50 percent of the 933,369 candidates. 909 Candidates have also been canceled for various reasons including fraud.

NECTA Executive Secretary Dr. Charles Msond said the leading National student is Grace Manga from Graiyaki Mara Primary School, followed by Francis Gwagi from Geita Paradise Primary School.

He said the third place winner was Loi Kitundu from Mbezi Primary School in Dar es Salaam, and Victor Godfrey from Graiyaki in fourth place.

"In academic performance, the Kiswahili, English and Science subject in the exam has improved and the subject in Mathematics has dropped,"

Primary School Leaving Examination (PSLE)
This is a selection test which enables the government to select form one entrants for its schools. Students who get selected and those who are not, receive certificates

How to check PSLE 2019 results online

Getting PSLE results online is just but a click away following technological innovation. The only requirement is a device capable of accessing the internet, more preferably a smart phone. Simply follow the steps listed below. Here’s how to check your PSLE 2019 RESULTS once it is declared.
  • Step 1- Visit these websites https://results.necta.go.tz/ or necta.go.tz
  • Step 2- Search for a tab saying PSLE Results 2019 Use this link https://necta.go.tz/psle_results
  • Step 3- Click it and on the new window Click find on page option on your browser and type your school name or number
  • Step 4- The PSLE Result 2019 will be displayed. Download or save the page and take a printout for future reference.

MATOKEO DARASA LA SABA 2019 SWAHILI VERSION

NECTA imeeleza ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.
Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde amesema mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi Paradise ya Geita. Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu ni Loi Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar es Salaam, na Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne. "Katika ufaulu wa masomo, somo la Kiswahili, Kiingereza na Sayansi katika mtihani huo ufaulu wake umepanda na somo la Hisabati umeshuka,"

Bofya link hizi kutazama matokeo ya darasa la saba

LINK 1>>>>>> https://matokeo.necta.go.tz/psle/psle.htm/ or necta.go.tz

LINK 2>>>>> https://matokeo.necta.go.tz/

Saturday, 27 April 2019

27 April

Ajira Mpya za Walimu 2018/2019


Ajira Mpya za Walimu 2018/2019

Ajira Mpya za Walimu 2018/2019, Ajira za Walimu 2018/2019,Ajira Mpya 2019   
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo 27 April 2019 Magogoni, Dar es Salaam, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Seleman Jaffo amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Serikali inawahudumia vizuri wananchi ameamua kufungua dirisha la ajira kwa walimu.

Jaffo amesema jumla ya waombaji 91108 wamejitokeza na kutuma maombi yao katika nafasi mbalimbali na kati ya hayo 43770 sawa na asilimia 48.04 yalikuwa na viambatanisho vyote vilivyohitajika.

Hata hivyo alieleza kuwa maombi 47338 sawa na asilimia 51.96 hayakuwa na vigezo ikiwa ni pamoja na kukosa viambatanisho muhimu vilivyohitajika.

"Kutokana na mahitaji makubwa kwa walimu katika shule za msingi na sekondari kwa masomo ya sayansi, Tamisemi imefanya uchambuzi na kutoa vipaumbele katika ajira za walimu daraja la tatu (A) cheti kwa ajili ya kufundisha shule za msingi. Walimu daraja tatu (B) stashahada wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kufundisha shule za sekondari( kidato cha kwanza hadi nne); na walimu daraja la tatu (C)shahada, wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kufundisha kwa kidato cha tano na sita," amesema Jaffo.

Pia walimu daraja la tatu (C) shahada, wa masomo ya elimu maalum, biashara, uchumi, kilimo na maarifa ya nyumbani kwa ajili ya kufundisha shule ya sekondari.

"Mchakato wa kupitia maombi ulijumuisha uhakiki wa uhalali wa vyeti vya elimu ya taaluma vya waombaji na ukamilishaji wa nyaraka zilizohitajika," amesema.

Aidha Jaffo ameeleza kuwa waombaji wa masomo ya sayansi na sanaa waliotimiza vigezo na hawakufanikiwa kupata nafasi kwa kipindi hiki, maombi yao yamechambuliwa na yamehifadhiwa kwenye kanzidata ya Tamisemi.

Amesema kwa walimu hao pindi fursa za ajira zitakapojitokeza utaratibu wa ajira utatolewa dhidi yao, "jumla ya walimu 4549 wamepangiwa moja kwa moja kufundisha shule zilizo na uhitaji wa walimu ambapo 3059 shule ya msingi na 1490 kwa sekondari".

Amewataka walimu wote waliopata ajira wanatakiwa kuripoti kwa wakurugenzi wa Halmashauri zenye shule walizopangiwa kwa ajili ya kuhakikisha vyeti vyao na kujaza mikataba ya ajira kisha kuripoti kwenye vituo vyao kuanzia Mei 7, mwaka huu.

Jaffo alisema walimu wapya ambao hawataripoti katika vituo vyao ifikapo Mei 21, 2019 nafasi zao zitajazwa moja kwa moja na walimu walio na sifa ambao hawakupangiwa bila kuwataarifu.

"Wakurugenzi wa Halmashauri wasikubali kubadilisha vituo vya kazi vya walimu bila kibali cha Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI. Walimu hawa tumewapangia kulingana na mahitaji ya sehemu husika".

Hatahivyo alisema kwa mwajiriwa atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kisha akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Thursday, 24 January 2019

24 January

Matokeo kidato cha nne | Form Four Results 2018/2019

Matokeo kidato cha nne | Form Four Results 2018/2019
Matokeo kidato cha nne | Form Four Results 2018/2019

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.


Wakati shule binafsi zikifanya vyema, mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo ni wa shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, Hope Mwaibanje.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma katibu mkuu wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).

Katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi.

Kutazama matokeo ya kidato cha nne 2018/19 bofya link zifuatazo;

Kindly use the following links to view NECTA CSEE Form Four Results (Matokeo ya Kidato Cha Nne 2018 / 2019 )Link 1: FORM FOUR NATIONAL EXAMINATION RESULTS 2018/2019

Link 2: FORM FOUR NATIONAL EXAMINATION RESULTS 2018/2019

QT Results – Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (QT) 2018

Matokeo ya Kidato Cha Nne 2018: Wanafunzi 10 Bora Kitaifa

Hope Mwaibanje ndiye mtahiniwa aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 yaliyotangazwa leo Januari 24, 2019 mjini Dodoma na katibu mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde.

Akizungumza na wanahabari leo, Dk Msonde amesema Mwaibanje wa Shule ya Sekondari Ilboru ndio amekuwa kinara akifuatiwa na Avith Kibani wa Marian Boys ya mkoani Pwani.

Walioshika nafasi ya tatu hadi ya sita wote ni wa shule ya sekondari ya St Francis Girls ya mkoani Mbeya ambao ni Maria Manyama, Atughulile Mlimba, Flavia Nkongoki na Leticia Ulaya.

Mwanafunzi wa saba na wa nane kitaifa ni Gibson Katuma na Bryson Jandwa (wote wa Marian Boys ya mkoani Pwani).

Idegalda Kiluba wa St Francis Girls ameshika nafasi ya tisa kitaifa na Isack Julius wa Marian Boys ya Pwani ameshika nafasi ya 10.

Kwa matokeo hayo, kati ya watahiniwa 10 bora kitaifa, watahiniwa watano ni wa Shule ya Sekondari St Francis Girls, wanne wa Shule ya Marian Boys huku Mwaibanje akiwa pekee wa shule ya Serikali ya Ilboru.

Kwa mujibu wa Dk Msonde, matokeo hayo yanaonyesha kuongezeka kwa ufaulu kwa watahiniwa kwa asilimia 1.28 kutoka asilimia 77.09 ya mwaka 2017 hadi asilimia 78.38 mwaka 2018.

“Takwimu zinaonyesha idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa daraja la kwanza hadi tatu imeongezeka. Mwaka 2016 ilikuwa asilimia 27.60, mwaka 2017 asilimia 30.15, na mwaka 2018 ni asilimia 31.76,” amesema Dk Msonde.

Matokeo ya Kidato Cha Nne 2018: Ufaulu Waongezeka
Baraza za Mtihani Tanzania (Necta) limesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018.

Dk Charles Msonde amesema ufaulu mwaka 2018 umefikia asilimia 78.38 ukilinganisha na asilimia 77.09 mwaka 2017.

Dk Msonde amesema somo la hesabu bado ni tatizo kwa wanafunzi kwani hata katika matokeo hayo ufaulu wa somo hilo ni asilimia 20.02 wakati somo la Kiswahili likiwa na ufaulu wa asilimia 89.32.

“Lakini hata kwa watahiniwa wa mtihani wa maarifa (QT) nako ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.35 lakini kwa ufaulu wa watahiniwa wa kujitegemea wenyewe ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.97 ikilinganishwa na mwaka 2017,” amesema Msonde

Katika mtihani huo, watahiniwa 322, 965 sawa na asilimia 78.38 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wamefauli, wasichana wakiwa 163, 920 sawa na asilimia 77.58 wakati wavulana waliofaulu wakiwa 159, 045 sawa na asilimia 79.23.

Mwaka 2017 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 287, 713 sawa na asilimia 77.09.

Matokeo ya Kidato Cha Nne 2018: Shule 10 Bora

St Francis Girls (Mbeya),
Kemebos (Kagera),
Marian Boys,
Ahmes,
Marian Girls (zote Pwani),
Canossa,
Bright Future Girls (zote Dar es Salaam),
Maua Seminari (Kilimanjaro),
Precious Blood (Arusha) na
Bethel Sabs Girls (Iringa).
Necta yafuta matokeo kidato cha nne sekondari ya Tumaini Lutheran
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.

Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24, 2019 na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.

Amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.

NECTA Form Four Results 2018 Grades

The quantification for grade ranges at SFNA results shall be as follows:-

 75 – 100 = A – indicating excellent
60 – 74 = B+ – indicating very good
50 – 59 = B – indicating good
40 – 49 = C – indicating average
30 – 39 = D – indicating satisfactory
20 – 29 = E – indicating unsatisfactory
0 – 19 = F – indicating fail
Matokeo Ya Kidato Cha Nne via SMS:
NECTA Tanzania National Examination Result : – allow students to check the “matokeo kidato cha nne” by sms through mobile. If you found your Internet connectivity is very slow then you may check the “matokeo kidato cha nne” using SMS, to get the result check the SMS process below.

Go to write message and type: matokeo*centre number*candidate number*exam type*exam year
Send SMS to 15311
Example:

matokeo*S21245*0013*sfna*2017
Send SMS to 15311
Get Rank Via SMS
Go to write message and type : rank*centre number*exam type*exam year
Send SMS to 15311
Example :

rank* S0131*sfna*2017
Send SMS to 15311
NB: Cost per SMS is Tshs 200/=

This service is only available for Tigo, Vodacom and Zantel subscribers.

NECTA Form Four Results 2018/2019 Online
From 2016 the National Examination Council Of Tanzania (NECTA) developed an online results system through their official website portal (www.necta.go.tz). Now students of Tanzania can check their result online. Check below for step by step guide to get the result online.


Matokeo ya form four 2018/ 2019 Online

Step 1 : visit www.necta.go.tz
Step 2: Find the “Result” in Main Menu and Click on “Search” from submenu.
Step 3: The “Search Result” window will appear shown in below.
Step 4: Select your “Year” as 2017
Step 5: Select “Exam Type” as SFNA.
Step 6: Enter Your “Candidate number” (SFNA)
Final Step: Click on “Request” button.
N.B.:

Do not forget to save/download the necta form four results 2017/2018 for future reference.

NECTA Contacts: The National Examinations Council of Tanzania
Address
The Execultive Secretary,
The National Examinations Council of Tanzania;
P.O. BOX 2624 OR 32019 ;
Tel: +255-22-2700493 – 6/9;
Fax:+255-22-2775966;
E-mail: esnecta@necta.go.tz
Website : http://www.necta.go.tz

Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017 / 2018
Matokeo ya kidato cha nne 2017 sasa yametoka
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.Certificate of Secondary Education Examination(CSEE)
Category: Matokeo ya Kidato Cha Nne
This is an achievement test offered to candidates who have completed four years of secondary education.

CSEE Examination Calendar
Category: Matokeo ya Kidato Cha Nne
CSEE is administered at the first week of November every year.

The objectives of CSEE
Category: Matokeo ya Kidato Cha Nne
The objectives of this examination are to assess students’ skills and knowledge achieved in different subjects at secondary school. Also to weigh the extent to which the student can use the skills gained to meet the social, political, economic and technological challenges for the individual and the national development at large; to identify students with the capacity to continue learning to the advanced secondary school level and other learning institutions. The holder of the CSEE qualification is expected to be able to apply skills of knowledge, comprehension, application, analysis, synthesis and evaluation in a broad range of activities.

Eligibility of Candidates who Seats for CSEE
Category: Matokeo ya Kidato Cha Nne
Any students who have completed four years of secondary education at both government and non-government registered schools and passed form two secondary education examination or Qualifying Test. Also, repeaters of the same examination who registered themselves as private candidates.

CSEE Examined Subjects/Courses
Category: Matokeo ya Kidato Cha Nne
The core and compulsory subjects that a candidate is registered to sit for CSEE are:


Civics,
History,
Geography,
Kiswahili,
English Language,
Biology and
Basic Mathematics.
Candidate may also sit for additional two subjects chosen from natural science subjects which are:

Physics and Chemistry or
Business subjects which are:
Commerce and Book Keeping;
Home economic subjects which are Food and Nutrition and Textile and Dress Making or
Technical subjects which are:
Building Construction,
Architectural Draughting,
Surveying,
Carpentry and Joinery,
Brickwork and Masonry,
Painting and Sign Writing, Plumbing,
Electrical Installation,
Electrical Engineering Science,
Radio and Television Servicing,
Electrical Draughting,
Refrigeration and air conditioning,
Plant and Equipment Maintenance,
Workshop Technology,
Motor Vehicle Mechanics,
Welding and Metal Fabrication,
Fitting and Turning,
Auto Electric,
Mechanical Draughting and Foundry and Blacksmith and
one optional subject among the following:
Bible Knowledge,
Elimu ya Dini ya Kiislamu,
Fine Art,
Music,
Physical Education,
French Language,
Literature in English,
Arabic Language,
Agricultural Science,
Information and Computer Studies and Additional Mathematics.
No candidate for the CSEE shall register for more than ten subjects at one sitting.

CSEE Examination Formats

Category: Matokeo ya Kidato Cha Nne
Each subject has an examination format which describes the structure of the examination paper, rubric and the content in which that particular examination covers. The details of subjects examined are shown in individual examinations formats that can be accessed in the examination formats link.