;
EDUSPORTSTZ : UWANJA WA MASTAA

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts
Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts

Friday, 25 May 2018

25 May

ZARI AWEKA WAZI HISIA ZAKE KWA IVAN DON

Pichani; zari na marehemu don wakiwa na familia yao
Ikiwa mwaka mmoja sasa umepita tangu kifo cha alikuwa mume wa zarithebosslady na moja ya watu waliounda kundi la rich gang ivan don.

Kupitia ukurasa wake wa instagram zari ameweza kuweka hisia zake na kusema kwamba hii wiki itakuwa na kwa ajili ya kumuenzi ivan kwa kumkumbuka yale ambayo walishea wote wakiwa pamoja.

zari ambae aliweza kupata watoto watatu wa kiume na ivan kabla ya kukutana na diamond ambae pia amemzalia watoto wawili na kufanya jumla ya watoto watano.

zari amesema kuachana nae hakumfanyi asimkumbuke kwani hakuna ubaya wowote aliufanya kwake na bado ataendelea kuwa kwenye kumbukumbu ya maisha yake kwani walifanikiwa kuwa wote katika maisha.
25 May

ALICHOKISHAURI NAPE LEO BUNGENI KWA MAWAZIRI WA JPM

 Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye, amewataka Mawaziri katika serikali ya awamu ya tano kuwa na tabia ya kusikiliza ushauri na kukubali kukosolewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye,

Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye, amewataka Mawaziri katika serikali ya awamu ya tano kuwa na tabia ya kusikiliza ushauri na kukubali kukosolewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.


Nape amesema hayo leo Mei 25, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kuchangia hoja mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na kuwataka Mawaziri hao kuiga mfano wa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu wake kwani ni watu ambao wanakubali kupokea ushauri.

“Wito wangu kwa Mawaziri wengine igeni mfano wa Kalemani, ukiambiwa jambo usilolipenda, wewe ni kiongozi kubali, sikiliza, mimi naamini Kalemani atakwenda vizuri, zipo changamoto kwenye Wizara yako, lakini ninaamini ukiendelea kuwa msikivu yale ambayo yapo juu ya uwezo wako mimi najua watu watakusamehe, lakini yale ambayo yapo ndani ya uwezo wako ukisikiliza na ukayatekeleza tutakuunga mkono” amesema Nape.

Mbunge huyo aliendelea kumwaga sifa kwa Waziri Kalemani kwa kufanikiwa kuiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara katika Gridi ya Taifa pamoja na kupeleka Meneja wa TANESCO katika Mkoa wa Lindi.

Kwa upande mwingine Nape ameishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuligawa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutenganisha majukumu ya uzalishaji na usambazaji na kutaka serikali kuingia ubia na sekta binafsi ili umeme uzalishwe katika kiwango kikubwa.

CREDIT TO EATV

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Tuesday, 22 May 2018

22 May

MASHARTI ALIYOYATOA BABA WA MAREHEMU KANUMBA KWA LULU

Baba Kanumba alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku chache baada ya mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa kujitokeza hadharani na kuoneshwa kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kubadilishiwa adhabu kutoka kifungo cha miaka miwili jela hadi kifungo cha nje.
Elizabeth Michael ( LULU)

MUNGU ametenda! Ndiyo maneno ya kwanza kutoka kinywani kwa baba wa aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Steven Charles Kanumba, Charles Kusekwa Kanumba mara baada ya kuanza mahojiano huku akieleza alivyofurahishwa na kitendo cha aliyekuwa mpenzi wa mwanaye, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kutolewa gerezani na kumpa masharti mazito mwanadada huyo.

Baba Kanumba alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku chache baada ya mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa kujitokeza hadharani na kuoneshwa kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kubadilishiwa adhabu kutoka kifungo cha miaka miwili jela hadi kifungo cha nje.

HANA TATIZO NA MTU

Tofauti na mama Kanumba ambaye alionesha kutaka Lulu abaki gerezani, baba Kanumba alisema kuwa, kutolewa kwa mrembo huyo ni mpango wa Mungu.

HUYU HAPA BABA KANUMBA

Baba Kanumba alisema kuwa, kwanza Lulu kutolewa gerezani na kubadilishiwa kifungo cha nje ni mpango wa Mungu na alifurahishwa mno na kutoka kwake hivyo kwenye moyo wake hana kinyongo naye hata kidogo.

“Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu na kila kinachotokea ni mapenzi yake, siwezi kulaumu kwa nini Lulu ametoka bali nimefurahi kwa sababu hata angefungwa miaka mia moja, Kanumba tayari alishafariki dunia, hawezi kurudi duniani.

MCHA MUNGU

“Silaumu kwa sababu mimi ni mcha Mungu hivyo Mungu ndiye amesema suala hilo lifikie tamati kwa namna hiyo, wanaopinga na kusema siyo haki, hayo ni mawazo yao maana kama ni kifo cha mwanangu kiliniuma sana, lakini sasa siwezi kumlazimisha Mungu afanye mimi binadamu ninavyotaka maana hata neno lake linatufundisha kwamba tusamehe,” alisema baba Kanumba.

AMPA MASHARTI MAZITO

Pamoja na kufurahishwa na suala la Lulu kutolewa gerezani na kupewa kifungo cha nje, baba Kanumba alimpa Lulu masharti mazito kwamba kama anataka maisha yake yaende vizuri, awe na familia nzuri kama watu wengine na amani moyoni, anatakiwa kwenda kufanya usafi kaburi la Kanumba kama ni kulia, alie na hapo atakuwa ameacha balaa na mikosi yote.

“Kwa mila za kabila letu la Kisukuma ni kwamba, Lulu alitambulika kama mke wa Kanumba maana hakuna mwanamke mwingine tunayemfahamu sisi hivyo natamani angeachiwa huru kabisa asiwe na kifungo cha nje na aende tu kufagilia kaburi la mumewe Kanumba na hapo atakuwa amemaliza na kuwa huru.

“Lulu kama anataka awe na familia, yaani aolewe, apate watoto wazuri na amani katika maisha yake, aende tu kufagilia kaburi la Kanumba na hapo atakuwa ameacha kila nuksi, balaa na mikosi hapohapo na atakuwa huru kabisa, ndiyo mila zetu zinavyosema,” alisema baba huyo.

ASIPOFANYA ITAKUWAJE?

Baba huyo aliendelea kueleza kuwa, endapo Lulu hatafuata na kufanya masharti hayo, basi atakuwa na wakati mgumu mno kwenye maisha yake kwa maana damu hiyo na mzimu wa Kanumba utakuwa ukimfuatilia na anaweza asiolewe au kupata familia, yaani watoto.

“Kinachotakiwa hapa, Lulu anatakiwa afuate tu hayo masharti ya kimila niliyompa, lakini asipofanya hivyo atajikuta akikosa amani katika maisha yake kwani kufanya hivyo kunamuepusha na kufuatiliwa na ule mzimu au damu ya Kanumba ambayo itamtesa na kujikuta akikosa furaha na amani,” alisema baba Kanumba.

MTU WA KARIBU ANENA

Mmoja wa watu wa karibu na familia ya Lulu ambaye aliomba hifadhi ya jina, alipotakiwa kuzungumzia masharti hayo ya baba Kanumba, alisema kuwa, familia imeyapokea na yanatekelezeka.“Kikubwa kwanza familia inamshukuru Mungu kwa kitendo cha kubadilishiwa adhabu ya gerezani na kumalizia kifungo chake cha nje.

“Unajua jambo lenyewe kama alivyosema baba Kanumba ni mipango ya Mungu tu. Familia haikutegemea kabisa kama Lulu anaweza kubadilishiwa adhabu.

“Unajua kama familia, baada ya hukumu ya miaka miwili kutolewa na Mahakama Kuu, Novemba, mwaka jana, licha ya kumuombea Lulu atoke, lakini kibinadamu tulikuwa tunajua ndiyo mpaka amalize miaka yake miwili gerezani ndiyo atoke,” alisema mtu huyo na kuongeza:

“Lilipokuja lile la msamaha wa Rais, nalo familia iliona tu ni kama Mungu anasikiliza maombi na kumpunguzia ile robo ya kifungo, lakini hakuna aliyekuwa anajua kwamba Lulu anaweza kutoka mapema hivi akiwa angali na miezi sita tu gerezani.”

MITANDAONI KWACHAFUKA


Mara baada ya Lulu kubadilishiwa kifungo hicho, mitandaoni kulichafuka kwa watu kumzungumzia mrembo huyo huku wengi wakionesha kufurahishwa na kitendo hicho.“Ni jambo la kheri sana. Lulu anapaswa kumshukuru Mungu kwa sababu sidhani kama alitegemea kama siku moja anaweza kutoka katika mazingira kama yale,” alichangia mdau mtandaoni.

Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii walisema kuwa, Lulu ni binti ambaye alikuwa ana msaada mkubwa katika familia yake hususan mama yake mzazi hivyo kitendo cha yeye kurudi uraiani kinaleta faraja kubwa.

Walisema kama mzazi, kitendo cha kutomuona mwanaye kwa muda mrefu kilikuwa kinampa mawazo na hivyo sasa ni wakati wa kuanza ukurasa mpya wa maisha ya furaha.

TUJIKUMBUSHE

Mwishoni mwa mwaka 2017, Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ilimuhukumu Lulu kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Kanumba, lakini Mei, mwaka huu mahakama hiyo ilimbadilishia adhabu na kumpa kifungo cha nje ambapo amekuwa akifanya kazi za kijamii kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar.

MCHANGANUO ULIVYOKUWA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Magereza, mfungwa yeyote (isipokuwa wa kunyongwa na kufungwa maisha) anapoingia tu gerezani anapata msamaha wa theluthi moja ya kifungo chake.

Hivyo Lulu alipoingia tu gerezani, alipata msamaha huo ambapo alipunguziwa theluthi hiyo na kubakiwa na miezi 16 badala ya ile 24 aliyohukumiwa mahakamani.

RAIS AMUOKOA

Baadaye, Rais Dk John Pombe Magufuli kupitia msamaha alioutoa Aprili 26, mwaka huu jijini Dodoma katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar aliwapunguzia wafungwa mbalimbali nchini robo ya vifungo vyao ambapo Lulu naye alinufaika na msamaha huo.

Hivyo kutoka kwenye miezi 16 iliyobaki, Lulu akabakiwa na miezi 12. Baadaye, Mahakama Kuu kupitia vipengele vya sheria, iliweza kumbadilishia kifungo Lulu baada ya kutumikia nusu ya kifungo chake yaani miezi 6.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. 

Monday, 21 May 2018

21 May

JE SUGU ANATAKIWA KUOMBWA MSAMAHA? MAJIBU YAKE HAYA HAPA

 Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amedai kwamba anatakiwa kuombwa msamaha kutokana na hukumu aliyopewa ya kutumikia kifungo jela bila sababu za msingi.
Joseph Mbilinyi

Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amedai kwamba anatakiwa kuombwa msamaha kutokana na hukumu aliyopewa ya kutumikia kifungo jela bila sababu za msingi.

Sugu amesema hayo leo Mei 21, 2018 katika viwanja vya Bunge Jijini, Dodoma ikiwa ni kikao chake cha kwanza cha bunge kuhudhria tangu ameachiwa huru baada ya kuhudumu kwa siku 73 katika Gereza la Ruanda, Mbeya, ameongeza kwamba bila kujali ni nani amempa msamaha lakini anastahili kuombwa msamaha kwa hukumu aliyopewa.

“Mimi naamini sikutakiwa kuwa ndani, na unapozungumzia suala la msamaha nabaki najiuliza, napewaje msamaha na mtu ambaye amekufunga, mtu ambaye wanasema ulimfedhehesha, kitu cha msingi sio nani kanipa msamaha, mimi siamini kana nastahili kupewa msamaha bali natakiwa kuombwa msamaha kwa kufungwa kiholela na kutoka kiholela” amesema Sugu.

Mbunge huyo ameongeza kuwa wafungwa pamoja na askari katika Gereza la Ruanda walishangaa kumuona mbunge huyo katika Gereza hilo, Sugu amesema “wafungwa na askari walinipokea vizuri, kwanza walishtuka sana kuona Mbunge ameletwa kwa kesi ambayo haileweki kwahiyo nilikuwa na kazi kama kiongozi ya kuwatuliza”  

February 26, 2018 Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya iliwatia hatiani Sugu na Emmanuel Masonga Katibu wa CHADEMA nyanda za juu kusini na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, lakini wawili hao waliachiwa huru Mei 10, 2018 kwa msamaha wa Rais Magufuli alioutangaza katika sherehe za sikukuu ya Muungano April 26, 2018.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ
21 May

WATAMBUE WALIOFUKUZWA CHADEMA LEO

  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama.
chedama yawafukuza uanachama watatu leo, may 21

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama.

Monday, 14 May 2018

14 May

SABABU ZILIZOFANYA JESHI LA MAGEREZA KUMUACHILIA LULU

Jeshi la Magereza limeeleza kuwa muigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameachiliwa Mei 12, 2018 kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuenda kutumikia kifungo chake nje ya gereza 'community service'
Jeshi la Magereza limeeleza kuwa muigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameachiliwa Mei 12, 2018 kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuenda kutumikia kifungo chake nje ya gereza 'community service'
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam na kusema kwa mujibu wa Sheria ya Magereza Sura ya 58 kifungu Na. 49 (1),(2)(3) mfungwa yeyote (isipokuwa mfungwa wa kunyongwa na wa maisha) mara baada ya kupokelewa gerezani hupata msamaha wa theluthi ya kifungo chake 1/3 ambapo Lulu alipata msamaha huo na alitakiwa kuachiwa huru Marchi 12, 2019.

Aidha, taarifa hiyo iliendelea kufafanua baadhi ya mambo kuwa katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Rais Magufuli kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa msamaha wa robo ya adhabu kwa wafungwa wote waliokuwa na sifa za kunufaika na msamaha huo.

"Kufuatia msamaha huo mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael naye alinufaika na msamaha huo na hivyo kutakiwa kutoka gerezani Novemba 12, 2018", imesema taarifa hiyo

Pamoja na hayo, taarifa hiyo imeendelea kwa kusema "kwa mujibu wa Sheria Na. 3 (2)(a) cha Sheria ya Huduma kwa Jamii ya mwaka 2002 wafungwa ambao vifungo vyao havizidi miaka mitatu hunufaika na utaratibu huo ambao unampa fursa mfungwa kutumikia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya shughuli au kazi zisizo na malipo kwa manufaa ya jamii. Mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, kutokana na kukidhi vigezo vya kisheria na kuonesha tabia njema akiwa gerezani amenufaika na utaratibu huo".


Muigizaji Elizabeth Michael alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mnamo Novemba 2017, kwa kosa la kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Friday, 11 May 2018