BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts
Showing posts with label UWANJA WA MASTAA. Show all posts

Thursday, 26 April 2018

26 April

BADNEWS- MAMA MZAZI WA LADY JAYDEE AFARIKI DUNIA

msanii wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee

Mama mzazi wa msanii wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, Bi. Martha Mbibo, amefariki dunia alfajiri ya leo .

Akithibitisha taarifa hizo kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, amesema kwamba mama yao amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Dabo amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu Jet jijini Dar es salaam, na familia itatoa utaratibu wa mazishi mara baada ya utaratibu wa kuupeleka mwili msanii wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee kuhifadhiwa kukamilika.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ

Tuesday, 24 April 2018

24 April

OFA YA CARLO ANCELOTTI KUFUNDISHA TIMU YAKE YA TAIFA YAANZA KUFIFIZA NDOTO ZAKE KUINOA ARSENAL

Carlo Ancelotti

Miongoni mwa makocha wakubwa Katika tasnia ya kabumbu waliokuwa wakipewa nafasi ya kurithi mikoba ya Arsene Wenger kocha aliye dumu Sana na  klabu ya Arsenal Carlo Ancelotti amepewa ofa ya kufundisha timu ya taifa lake la kuzaliwa la Italia.

Kocha huyo "Ancelotti" ni miongoni mwake makocha wa zamani Katika timu za AC Milan, PSG, Chelsea na Real Madrid. 

Ancelotti alikaririwa akisema kwamba kuhusishwa kwake na Arsenal ni jambo ambalo linamfurahisha na baadhi ya mashabiki wa Arsenal walikuwa wanampigia kampeni apewe majukumu katika klabu yao. 

Mamilion ya mashabiki na wapenzi wasoka duniani wanasuburiwa kuona kocha Ancelotti kama ataamua kubeba majukumu ya Italia au asubiri ofa ya Arsenal.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Monday, 23 April 2018

23 April

KIFO CHA MSANII JEBBY CHA WAGUSA WATANZANIA

Jebby enzi za uhai wake


Msanii wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Jebby ambaye amewahi kufanya vyema na wimbo kama Swahiba amefariki dunia jana April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Watu wa karibu na msanii Jebby wamesema kuwa msanii huyo alikuwa anaumwa na mpaka umauti umemkuta Dodoma alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya bandama na ndiyo yaliyosababisha kifo chake.


Msanii Afande Sele pia amethibitisha hilo na kusema kuwa Jebby alikuwa anasumbuliwa na matatizo hayo ya bandama na kuwa jana ndiyo amefariki dunia.

"Hayupo tena duniani swahiba...pumzika kwa amani mdogo wangu wa haki Jebby.Tukimaliza kazi tutavalishwa taji" alisema Afande Selle

Credit to malunde1blog
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Sunday, 22 April 2018

22 April

KILIO CHA WATANZANIA KWA TCRA NA SERIKALI KUHUSU SHERIA MPYA YA USAJILI NA TOZO KWA MITANDAO

Sheria mpya na gharama za usajili na tozo kwa shughuli za mitandaoni zinazohusiana na blogs, website, forums, YouTube, TV na radio imeleta majonzi kwa watanzania na wamiliki wa mitandao hiyo ambao kwa kiasi kikubwa ni vijana wa kipato cha chini waliojiajili kulingana na ugumu wa ajira nchini.
Kwaniaba ya watanzania na bloggers, BakalemwaTz chini ya mwamvuli wa Tanzania Bloggers Association (TBA) anatoa machojizi yake kwa serikali na mamlaka husika kuokoa wimbi la vijana hawa wanaoelekea kupoteza mwelekeo wa kimaisha kulingana na sheria hii Mpya.

Anaandika kwa kusema haya:-
Binafsi nipende  kuchangia kidogo juu ya sheria mpya ya usajili na ulipiaji wa huduma ya online content kwa blogs, website, YouTube channels na huduma nyinginezo zihusuzo online content service. 

Niwazi kuwa serikali yetu ya Tanzania kwa jicho la pekee imeona kuwepo kwa umuhimu wa kufanya jambo hili ikiwemo kudhibiti utoaji wa Taarifa za uongo, uchochezi na uvujishwaji Siri za serikali, uvunjifu wa amani ya nchi,  utoaji wa maudhui machafu na yenye lengo la kuharibu utamaduni wa kitanzania n.k.

Nchini Tanzania mapinduzi ya kiteknolojia juu ya huduma ya utoaji wa habari mitandaoni umeanza miaka ya 2005-2007. Mapinduzi haya yaliwawezesha watanzania kupata habari kwa wakati, kupanua huduma za masoko ya biashara, huduma ya elimu bure kwa wanafunzi mitandaoni, huduma za kiroho kwa dini,  huduma ya Taarifa za schoolarships kwa wanafunzi kusoma nje na ndani ya Tanzania, Taarifa juu ya fursa za utalii na serikali zilizopo nchini.

Licha ya kuwepo kwa Taarifa zisizokuwa na maudhui na ueredi mitandaoni, huduma hii husaidia mamilioni ya watanzania kupata habari kwa wakati na muda muafaka. *Mfano* : miaka ya nyuma serikali ilipo kua ikitoa matokea ya kidato cha nne necta ilikua ni tabu kupata matokeo hayo kwa wakati kwani ilikua inachukua mpaka siku zaidi ya saba mtu ajaona matokeo yake,  hii ilitokana na 

*1:Uwepo wa mitandao michache*(blogs,forums na websites):- hivyo ilipelekea kuwepo Taarifa chache mitandaoni, hivyo ilikua ni vigumu kupata Taarifa kwa wakati kipindi hivyo. 

2:Traffic jam:- Kutokana na idadi kubwa ya watu online at once.Hivyo mapinduzi haya yalileta faraja kwa mamilioni ya watanzania walio wengi.


Ni jambo lisilofichika kuwa mamilion ya watanzania, serikali na makampuni Binafsi wamefaidi kwa kiasi kikubwa uwepo wa wingi wa mitandoo hii kwani umeifanya Tanzania kuwa kijiji na kuitangaza Tanzania nje ya nchi, hivyo imekua ni kituo cha taarifa za utarii na fursa zilizopo nchini.

 *Kwa nini kufungiwa kwa mitandao na kuwepo kwa sheria hii!?* 
 Ikumbukwe Rais Xi Jinping wa China alipoulizwa kwanini kumekuwepo na wingu la kufungia mitandao alijibu "mitandao imeleta Shida kubwa katika utawala wa nchi, ulinzi pia na maswala yetu ya maendeleo" kwahiyo walifanya hivyo kwa sababu kuu 3:

1: Kutoa fursa kwa mitandao ya ndani

Hii ilikua moja ya sababu kuu nchini humo, licha ya kuwepo sheria kali, hakukuwepo tozo na ushuru kwa mitandao ya ndani ili kuruhusu ushindani wa bidhaa na technolojia ya ndani kwa ajili ya Kukuza kipato cha nchi. Ni kweli kwamba nchini China hakuna mitandao Kama YouTube, what's App, na facebook na badala yake wanatumia mitandao Kama Baidu kama google,  wechat badala ya what's App Meipai badala ya instagram na youku Kama mbadala wa YouTube 

 2:Kulinda sera na maudhui ya nchi

Serikali ya China Iliona haina uwezo wa kuzuia uchangiaji juu ya masuala ya kisiasa na ukosoaji wa serikali na kuamua kufungia mitandao ya nje ya nchi ili kuweka self regulation kwa mitandao ya ndani. 

 3:Udhibiti wa maudhui yasiyo na maadili .

Hii ilikua ni kwa ajili ya kuisaidia serikali kuweka pin kwa site za nje ya nchi zenye maudhui yasiyoendana na utamaduni wao.


 OMBI KWA TCRA NA SERIKALI


Ndugu waheshimiwa viongozi wetu wa TCRA na Serikali, nikiwa miongoni mwa watanzania na bloggers wenye mapenzi mema na Tanzania naomba mtusaidie mambo haya yafuatayo kwa faida ya maendeleo ya taifa Letu.

1: Kuondolewa kwa tozo juu ya usajili wa blogs, you tube channel, website n.k

Hii itasaidia ukuaji wa technolojia ya mawasiliano nchini na kuruhusu uwepo wa stock ya Taarifa, documents na files kwa ajili ya kizazi kijacho. Pia itasaidia maelfu ya watanzania kujiajiri kwani huduma hii Mara nyingi hutolewa na vijana ambao ni tegemezi kwa taifa na familia.


2:Kuwepo kwa system yenye uwezo wa kuchuja nakuondoa maudhui yasiyofaa


Hii Itakua mbadala wa kublock na kufilt contests zenye lengo la kuharibu amani ya nchi pamoja na utamaduni wa nchi.


3:Kutoa ruzuku kwa blogs, you tube channels, forums,   (online content platforms )zisizo za kibiashara

Niwazi kuwa zipo online content zilizoanzishwa kwa malengo ya kutoa elimu na huduma Katika jamii na nyinginezo zikiwa ni za mashule, afya, pamoja na mashirika mbali mbali ya maendeleo Katika jamii hivyo wengi wao hawatakua na uwezo wa kumudu gharama hizo kwani huduma zao ni bure.

4:Kuanzishwa kwa ushindani wa technologia za mawasiliano za Tanzania


Hii itasaidia kupromote technolojia ya ndani na kukuza kipato cha nchi. Nyongeza ya hapa nikwamba database yake itakua rafiki na sera ya nchi pamoja na tamaduni zetu.   

5:Kutoa leseni za utambuzi kwa blogger Kutoka TRA


Niombe serikali iwape kibali TRA kutoa vibali kwa waendeshaji wa mitandao yote nchini ili kuendesha shughuli nzima chini ya sheria husika za mamlaka hii. Katika kipengele cha makadirio ya malipo ya ushuru niwazi kuwa kuna site maalumu
Mtandaoni zenye uwezo wa kukadiria kipato na thamani ya online content platform yeyote, hivyo itawarahisishia TRA Katika utoaji wa leseni za uendeshaji wa huduma hiyo pamoja na utozaji wa kodi kwa maendeleo ya taifa Letu. 

Mwisho: Nimalizie kwa kusema msemo huu wa kiswahili "vita ya panzi ni furaha ya kunguru" nikiwa na maana kwamba serikali na taasisi husika inabidi viwe makini na wamiliki wa mitandao hii wenye kipato kikubwa kwani watataka kupewa kipaumbele ili kudhibiti ukuaji wa ushindani Katika technolojia mawasiliano na kuwaacha maelfu ya watanzania bila ajira pamoja na kuminya upatikanaji wa Taarifa kwa wakati. Vivyo hivyo inaweza kupelekea upenyaji wa makampuni makubwa kutoka nje ya nchi kuendesha hudumu hizi kwa gharama za juu kuliko ilivyokua awali kwa lengo la kurejesha fidia ya undeshaji mzima wa mitandao hiyo. 

Nimatumaini yangu serikali yetu tukufu chini ya Rais John Pombe Magufuli itafanyia mabadiliko sheria hii mpya kwa kuondoa tozo hii na kuweka njia mbadala kunusuru na kudhibiti ukuaji wa tasnia ya technolojia mawasiliano na uhuru wa kupata habari kwa urahisi.

 Na BakalemwaTz mwakilishi kutoka www.edusportstz.com

Nakupenda Tanzania 
 MUNGU IBARIKI TANZANIA.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:
Delivered by EDUSPORTSTZ

Friday, 20 April 2018

20 April

HII HAPA TAARIFA YA KIFO CHA MASOGANGE NA WASIFU WAKE

Agnes Masogange 

Taarifa zilizotufikia hivi punde ndani ya www.edusportstz.com zinadhibitisha kwamba Video Vixen maarufu nchini Agness Masogange amefariki dunia mchana huu wa leo April 20, 2018.

Chanzo cha kifo hiko ni baada ya presha kupanda ghafla mpaka kupelekea kulazwa hospitali na kufariki.

Kifo chake kimetokea katika hospitali ya Kwa Mama Ngoma iliyopo mwenge jijini Dar es Salaam aliokuwa anapatiwa matibabu.

Masogange alizaliwa tarehe 8, September mwaka 1989, akiwa na miaka 20s alijishughulisha na maswara ya urembo akiwa Kama video vixen na alimewahi kuchukua tuzo ya wanavideo vixen bora nchi kwa mwaka 2009, 2011, 2012.

Masongange alijipatia umaarufu kupitia kibao Chake bele9 kiitwacho "masogange" kilichitamba miaka ya 2011-2012

Awali mwa mwezi wa nne masogange alipatikana na hatia ya matumizi ya madawa ya kukevya Aina ya Heroin na Oxazepam.  Hukumu hiyo ilimtaka atoe faini ya 1.5Million au kifungo cha miaka 3. Masogange alitoa kiasi hicho na kuachiwa huru mnaomo tarehe 03 April mwaka huu.

Edusportstz inatoa pole kwa wafiwa wote na familia ya marehemu 

Wednesday, 18 April 2018

18 April

MANENO YA ZITO KABWE BAADA POLEPOLE KUMKOSOA KUHUSU UPOTEVU WA 1.5T


Mhe Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Maendeleo
Zitto kabwe Mbuge wa Jimbo la kigoma mji na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo kupitia ukurasa wake wa twitter na facebook amejibu hoja za katibu wa itikadi na uenezi wa CCM humphrey polepole aliyesema zitto kabwe anapotosha UMMA juu ya tuhuma za upotevu wa trion 1.5 kulingana na repoti ya CAG Kama anvyo dai Mh Zitto Kabwe.

Polepole pia amesema kuwa Zitto kabwe ana bahati kwa kua rais JPM ni mpole vinginevyo angekua ameisha chukuliwa hatua kwani alizoeshwa vibaya. Pia amesisitiza kuwa anapaswa kuchukuliwa hatua kwani anapotesha repoti ya CAG


Zitto Kabwe ame yaandika haya
Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG.
Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO.
Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo ( mawazo yangu hayatakufa).
Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie.
Pia Zitto ameendelea kusisitiza kuwa anao uzoefu wa kutosha wa miaka 8 akitumikia PAC na POAC hivyo nidhahiri ya kuwa trioni 1.5 ya watanzania haina maelezo ya matumizi yake. 
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
18 April

POLEPOLE ALIAMSHA DUDE-AITETEA REPORT YA CAG KWA KUMVAA ZITTO PAMOJA NA UPINZANI
Katibu wa Itikadi na uenezi CCM, Humphrey Polepole anaongea na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya CAG

Polepoele anasema kuna viongozi wa vyama vya siasa wanapotosha ripoti hiyo na inafaa iwekwe utaratibu waanze kuchukuliwa hatua

Polepole amesema kuna kiongozi mmoja wa upinzani amekuwa akizungumza uwongo na kuleta taharuki kwa wananchi na kusema inafaa achukuliwe hatua ili aach

Polepole amesema anaipongeza serikali ya CCM kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuweka hadharani ripoti ya CAG na kuchukua hatua kwa wanaofanya ubadhirifu unaobainishwa.

Polepole anaipongeza serikali kwa kuwa Rias Magufuli alipochukua hatua za awali, mawaziri nao walifuta hatua hizo na kuwachukulia hatua maafisa kwenye wizara zao

Polepole amesema pia vipo vyama vya siasa vinatumia fedha ya umma na havitoi hesabu na kusemainabidi vichukuliwe hatua kali za kinidhamu


Amesema vipo vyama vimetumia zaidi ya Sh. milioni 700 bila kutoa hesabu, pia vipo vyma ambavyo vinatumia fedha bila kufuata kanuni za kihasibu

Kuna chama kinaitwa ABC, SAU, CHADEMA wametumia fedha bila kutoa hesabu zilivyotumika na pia kutumia fedha zaidi ya bilioni 2.2 bila kupeleka benki na kuhoji vinawezaje kuikosoa serikali?

Pia CHADEMA imefanya manunuzi ya zaidi ya bilioni 24 bila kushindanisha wakati ndio hao wanaoisema serikali


Polepole anasema isiidhie kuwataja kwenye taarifa ila msajili achukue hatua, hata kama ni ndani ya CCM


Polepole amesema inapotoshwa kuwa CCM imekopa ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii, CCM ina utaratibu wake wa ndani wa kulinda maslahi ya watumishi wake tofauti na vyama vingine


CCM ina utaratibu wa kulimbikiza fedha kila mwisho wa mwezi ili watumishi wake wanapomaliza utumishi, ipo fedha ya kuwalipa mafao yao

Katika akaunti ya CCM inayosimamiwa na Baraza la wadhamini walitoa zaidi ya milioni 300 ili watumishi wanaaondoka walipwe na wanazirudisha ili mfuko uendelee kunona

Amesema CHADEMA wamepotosha juu ya hili na wanapaswa kuchukuliwa hatua

Polepole pia anasema serikali ya CCM sasa ina utaratibu wa kuweka hesabu za serikali katika mtindo jumuishi, zamani zilikuwa zikitolewa kwa wizara na taasisi moja moja lakini kwa sasa unaweza kuzipata katika sehemu moja

Tanzania ni nchi ya pekee kufanya hivyo katika Afrika Mashariki na hii inasaidia kuweka mambo wazi zaidi na mtindo huu ni mgumu

Polepole amesema Zitto Kabwe ndio anaongoza kupotosha ripoti ya CAG kwa kukurupuka naripoti asizozielewa, na kusema Taarifa ya CAG ilikuwa imeshapitiwa na wao kwanza

Polepole anasema anapotosha kuwa trilioni 1.5 zimepotea na kufafanua kuwa sasa kuna mtindo mpya ambao unafuata vigezo vya kimataifa vya ukaguzi wa hesabu za umma unaitaka serikali inapokagua fedha zake zinapoingia kuhesabu pia na pesa baada ya serikali kuwa imetoa huduma ,
zamani ilikuwa ni lzaima ipokee fedha kwanza ndipo ihesabu fedha imeingia, ila sasa huduma inapotolewa hata kama fedha haijakusanywa inahesabiwa (acrrual basis)

Makusanyo ghafi ni makusanyo ya jumla, baada ya makusanyo ghafi inatakiwa ukokotoe ujue makusanyo sahihi ni yapi

Tumekusanya trilioni 25.3, pesa ambayo huduma imetolewa na inatarajiwa imekushwa kuingizwa kwenye jumla hiyo

ukitaka kujua makusanyo halisi unachukua trilioni 25.3 unatoa makusanyo tarajiwa (receivables)


Unachukua trilioni 25.3 unatoa bilioni 687.3 (receivables) kama hatua kupata makusanyo halisi

Pia unatoa bilioni 203.92 ambazo ni fedha zilizokusanywa kwa ajili ya Zanzibar, ambayo haisomwi kwenye bajeti ya Serikali ya Muungano

Ukitoa hesabu hizo unapata Shilingi trilioni 24.4 hizi ndio makusanyo halisi ya mwaka 2017/208

Zitto anadai pesa zilizotumiaka kutoka trilioni 25.3 ni trilioni 23.79, hii kipindi mkaguzi anapita zilikuwepo fedha za serikali ambazo zilikuwa kwenye hatifungani (zilikuwa hazijaiva) ambayo ni shilingi 697.85 bilioni

Ukichukua 697.85 bilioni ukijumlisha trilioni 23.5 unapata trilioni 24.4, na ukichukua 25.3 ukatoa 23.79 unapata 1.5 trilioni ambayo ndio zitto anadai imeibiwa

Polepole anasema Zitto hajui hesabu na anapaswa kumtafuta mwalimu.

Polepole anasema pia Zitto amepotosha kuhusu bilioni 219 ambayo ililipa madeni ya zamni ambayo hayakuwa yamepitishwa na Bunge

Amesema haesabu za serikali zinawekwa kwenye vifungu, na kulikuwa na madeni ya watu mbalimbali yanayofikia bilioni 969 ambayo yalipitishwa na Bunge na serikali inayalipa baada ya kuyahakiki, bilioni 219 ni sehemu ya bilioni hizo 969 zinazofahamika na Bunge pia

Polepole amesema Zitto amepotosha pia kuhusu serikali kukopa bilioni 500 ambazo ni zaidi ya ukomo iliyowekewa, amsema hili hatajibu analiachia Bunge, hayo mawili ameyazungumzia ili kumpa elimu


Polepole amesema Zitto achukuliwe hatua kwa kupotosha na ni kwa sababu alikuwa amezoeshwa vibaya.

WEKA EMAIL YAKO HAPA KUTUMIWA HABARI


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
18 April

BADNEWS-MKE WA RAIS MKONGWE HW BUSH AFARIKI DUNIABarbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92.

Ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo akiwemo mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush.


Bi Bush ambaye alikuwa mke wa rais kutoka 1989 hadi 1993 amekuwa akidorora kiafya kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi.


Risala za rambirambi zimetumwa nchini Marekani kutoka maeneo tofauti duniani.


Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani.

Barbara Bush na mumewe aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush


Mwana wao George alichaguliwa 2000 na kuhudumu kwa miula miwili kama rais wa 43 wa Marekani.


Katika tanzia alisema katika taarifa yake kwamba ''mamangu mpendwa ametuwacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura Barbara, Jenna na mimi tunaomboleza , lakini roho zetu zimepumzika kwa sababu tunajua yake pia imepumzika.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.


WEKA EMAIL YAKO HAPA KUTUMIWA HABARI :
Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Thursday, 12 April 2018

12 April

MANENO YA LOWASSA KUHUSU KUPIMA DNA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa pichani na binti anayesemekana alimzaa na kumtekekeza


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hamtambui mwanamke aliyejitambulisha juzi kama binti yake aliyetelekezwa na kwamba hatapoteza muda kwenda kupimwa vinasaba (DNA), kama msichana huyo alivyotaka.

Kwa mujibu wa mazungumzo na Gazeti la Nipashe, Lowassa ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema kuwa kinachofanyika kwenye zoezi hilo ni siasa.

Msichana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma alijitokeza hadharani juzi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kudai kutelekezwa na Lowassa ambaye alisema ni baba yake, kwa kuambiwa na mama yake mzazi.


"Wewe unamwamini kweli huyo msichana? Angekuwa mwanangu kweli ningeshamchukua muda mrefu, kwanza wala simjui naona siasa zinaingizwa hapo," alisema.

Alipoulizwa kama yuko tayari kupimwa DNA ili ukweli ujulikane, Lowassa alijibu "Kupima DNA huo ni upuuzi. Yaani nipoteze muda wangu kwenda kufanya upuuzi huo? Siko tayari."

Msichana huyo ni miongoni mwa mamia ya wanawake waliojitokeza kuanzia Jumatatu kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.

Makonda alitaka wanawake waliotelekezewa watoto na waume zao wafike ofisini kwake kwa siku tatu kuanzia Jumatatu, kwa ajili ya kuzungumza na wanasheria, maofisa wa ustawi wa jamii na askari polisi wa Dawati la Jinsia. Siku hizo zitaisha kesho baada ya kuongezwa.

Akizungumza na vyombo vya habari juzi, Fatuma alisema yuko tayari kupima vinasaba na Lowassa ili kuthibitisha kama kweli ni baba yake na kwamba alimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.

"Nilipeleka barua Ikulu kuomba kuonana na baba (Lowassa) kipindi akiwa Waziri Mkuu (2006-2008) lakini niliitwa mimi na mama katika klabu ya Mamba iliyopo Kinondoni," alisema Fatuma.

"(Hapo) alikuja mwanaume akiwa kwenye gari lenye vioo vyeusi akatuhoji mimi na mama, akaondoka hakutupa majibu yoyote hadi leo."

Kuhusu madai hayo, Lowassa alisisitiza kuwa kama kweli angekuwa mtoto wake asingesita kumchukua.

"Wala simjui, anasema ameshindwa kuniona wakati ana miaka 31, wewe unaamini kweli ameshindwa kuniona? Mbona wewe umenitafuta na umenipata na unaongea na mimi kwenye simu," alisema Lowassa.

"Hizo ni siasa zinazolenga kuchafuana."

Pia katika maelezo yake, Fatuma alidai kuwa aliwahi kukutana na mtoto wa Lowassa aitwaye Fred na alimwahidi kumsaidia lakini hadi sasa amekuwa kimya.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Monday, 9 April 2018

09 April

ALICHOKIZUNGUMUZA NAPE NNAUYE LEO BUNGENI

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
WEKA EMAIL YAKO HAPA KUTUMIWA HABARI


Delivered by EDUSPORTSTZ
Mbunge Wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, Amesema Kuwa Wapiga Kura wa Mikoa Ya Lindi Na Mtwara Walitegemea Kupata Neema Kubwa Kutokana na miradi Ya Gesi, na ndiyo Jambo Ambalo walilipa kipaumbele katika ilani ya chama cha Mapinduzi. Mbunge Nape amesema kuwa ameshangaa kuona kuwa Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, hajalizungumzia kabisa suala hilo kwenye hotuba yake ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu aliyoiwasilisha bungeni.

Bofya hapa kutazama  video hiyo
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Chanzo. Globalonlinetv

Sunday, 8 April 2018

08 April

WAJUE MISS TANZANIA WANAHARAKATI

Mashindano ya ulimbwende ni mlango wa fursa

Miss Tanzania wa zamani waiambia BBC namna ulimbwende ulivyofungua milango ya fursa za kibiashara na huduma kwa jamii
Miss Tanzania ,2005

Anafahamika zaidi kama Miss Tanzania na Miss World Africa wa mwaka 2005, lakini leo hii mlimbwende huyu ni mjasiriamali na mwanaharakati wa kijami aliyeamua kuwainua vijana na wanawake zaidi katika nyanja mbalimbali za kijami.

Nancy Sumari, ni mfanyabiashara ambaye anamiliki kampuni ya habari kwa njia ya mtandao iitwayo 'bongo5'. Anasema mtandao huu wa habari unalenga kumjenga kijana kimawazo ili aweze kufanya maamuzi sahihi kwa kumpa habari na burudani.

Mbali na kampuni hiyo anamiliki pia taasisi ya mafunzo ya tehama kwa watoto inayochapisha mfululizo wa vitabu viitwavyo Nyota .
Nancy Sumari akizindua kitabu chake cha hadithi na mashairi kwa watoto

Shughuli hizi anazozifanya anasema zinampa fursa ya kujihusisha zaidi na miradi ya kuwawezesha wanawake, kutoa mafunzo kwa vijana na kusaidia katika kuboresha elimu nchini.

Taji la ulimbwende kwa Sumari, ni jambo ambalo anajivunia sana kwa sababu limempa fursa ya kukutana na watu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali duniani na vilevile kutembea maeneo mengi duniani.

Anasema mashindano ya Miss Tanzania, ni jukwaa zuri ambalo linamjenga mtu kwa kile ambacho amelenga kukipata ingawa huwa inategemea na mtu mwenyewe na nini anataka kufanikisha.

Nancy anaamini kwamba sio kila kitu ambacho unaweza kukiona kwenye mtandao ndio uhalisia, kuna kazi kubwa nyuma ya pazia.

Mwaka 2017, Sumari aliweza kupata tuzo la vijana 100 wenye ushawishi zaidi Afrika, lifahamikalo kama 'Africa Youth Awards'.
Baadhi ya wajasiriamali waliowahi kuvikwa taji la Miss Tanzania

Yeye pia ni mjumbe wa World Economic Forum, Mandela Washngton Fellow.
Nasreen Karim,Miss Tanzania 2008

Mbali na Nancy wapo walimbwende wengine walioenda mbali zaidi na kujivika mataji ya ujasiriamali na kujihusisha na shughuli zingine za kijamii.
Nasreen Karim, alikuwa miss Tanzania mwaka 2008. Kwa sasa yeye ni mjasiriamali na mkurugenzi wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Enjipai Masai women foundation, inayoshughulika na kazi za utamaduni na sanaa ambazo anawashirikisha akina mama wa kimasai.

Biashara anayofanya alianza mara tu baada ya kumaliza muda wake wa Miss Tanzania.

Aliamua kuanzisha biashara hii kwa madhumuni ya kuwainua akina mama ambao wanajishughulisha na ubunifu wa shanga kwa kutengeneza vitu mbalimbali vya urembo .

"Nilipata wazo hili wakati nikiwa miss Tanzania, na liliweza kunipa fursa nzuri ya kushinda tuzo ijulikanayo kama 'Beauty with purpose' 'jambo ambalo niliona ni muhimu kuliendeleza."

Nasreen anasema kwa mwaka mmoja ambao alikuwa karibu na jamii akiwa miss Tanzania kulimuwezesha kugundua kwamba kuna umuhimu wa kuendelea kuwa karibu na jamii.
Mjasiriamali wa bidhaa za utamaduni,Miss Tanzania 2008

Katika hiki anachokifanya leo, anaona kama sehemu ya muendelezo wa pale alipoishia wakati akiwa miss Tanzania. Anasema anajivunia kwamba shughuli zake za kijamii anazozifanya sasa ndio zinazomtambulisha zaidi .

Nasreen anaamini kwamba mashindano ya ulimbwende ni fani kama fani nyingine na inampa mtu muda mfupi sana wa mwaka mmoja ambao kama mtu ana malengo atafanikiwa kwa sababu ya jukwaa kubwa kutoka kwa vyombo vya habari na makampuni mengi yanayotaka kumtumia kwenye matangazo na kumuunganisha kwa watu wengi duniani.
Miss Tanzania 2012,amejikita katika kuwawezesha watu wenye ualbino

Anasema hivi sasa shanga za kimasai ni bidhaa ambayo ina wateja wengi duniani kote na ina mvuto wa kisasa.
Brigete Alfred, msichana mwenye umri wa miaka 23, alipata taji la ulimbwende wa Tanzania mwaka 2012 akiwa na miaka 18.

Yeye amemaliza chuo kikuu mwaka jana, ambapo alikuwa anasomea Uchumi na masoko. Vile vile ni mkurugenzi wa asasi isiyokuwa ya kiserikali inayoitwa 'Empowering margnalised group' inayosaidia watu wenye ualbino nchini Tanzania.

Brigite alipata nafasi ya miss Tanzania kipindi ambacho nchi ilikuwa ina janga kubwa la kujeruhiwa na hata kuuwawa kwa watu wenye ualbino hivyo shughuli nyingi za taji lake zilimuhamasisha yeye kuwa karibu zaidi na jamii hiyo.

Shughuli hizo pia zilimpa fursa ya kuwa mshindi wa tatu katika kipengele cha 'Beauty with Purpose' katika mashindano ya dunia.

"Jukwaa hili la Miss Tanzania lilinipa fursa ya kujionea na kujua ni nini kinakosekana katika jamii yangu, sina uwezo mkubwa sana lakini kwa kidogo nilichonacho ninajivunia kuwa nimemuwezesha kijana mwenye ualbino kuweza kulala katika nyumba salama baada ya kuwajengea bweni la watoto 300 huko shinyanga"

Brigite anaamini kuwa kama asingekuwa miss Tanzania basi asingeweza kuwa na maono mazuri kama haya, anasema hakuna ambaye aliyemshawishi kufanya chochote ila nafasi hiyo ilimpa fursa ya kufikia hicho anachokifanya.
Miss Tanzania 2008,Brigitte Alfred

Lakini vile vile anajivunia kupitia kampuni yake anaweza kumpa mafunzo kijana mwenye ualbino ambaye hajawahi kwenda shule kuweza kujua namna ya kutunza fedha katika akaunti, kujiajiri, kufanya biashara ndogo ndogo na kuanzisha vikundi vya kukopeshana na kujua namna ya kujikimu kimaisha.
Wasichana wengi wanapata taji la miss Tanzania wakiwa na umri mdogo na ni wakati ambao unaweza kujijenga au ukapotea, anasema Brigitte.

Hata hivyo anaonya kwamba kama mtu hana watu wa karibu wa kumuunga mkongo ni ngumu kufanikiwa na kutumia fursa iliyopo mbele yao.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Thursday, 5 April 2018

05 April

ROMA AKABIDHIWA RASM CHETI NA BASATA-AFUTA WIMBO WA KIBAMIA

Rapa Roma Mkatoliki, akikabidhiwa cheti cha usajili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata

Rapa Roma Mkatoliki, akikabidhiwa cheti cha usajili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mungereza, baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

RAPA Roma Mkatoliki, leo Alhamisi amekabidhiwa cheti cha usajili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ili aweze kufutiwa adhabu yake ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar, Ibrahim Mussa’ maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki aliwashukuru watu wote waliopaza sauti hadi kufutiwa adhabu hiyo, huku akiwaasa wasanii wenzake kuchukua hatua mapema za kujisajili.

Aidha Roma alisema kuwa, kitendo cha wimbo wake wa Kibamia ni sawa huku akivitaka vyombo vya habari kuacha kuupiga wimbo huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mungereza (kulia) akizungumza jambo.

Rapa Roma Mkatoliki akiwa katika ofisi ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).
Chanson.: globalpublishers
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Thursday, 29 March 2018

29 March

MWAKYEMBE AMFUTIA ADHABU ROMA KWA SHARTI HILI
Wizara ya Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni imemfutia adhabu Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo Roma Mkatoliki iliyokuwa imempatia kutokana na wimbo wake wa Kiba 100 kukosa maadili.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jioni, Waziri Mwakyembe amesema kwamba Wizara imeamua kumfungulia msanii huyo baada ya kukiri kuwa amefanya makosa na kuahidi kwamba atakuwa balozi wa maadili.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa msamaha wa msanii huyo utaanza mara moja pale ambapo msanii huyo atakapo kamilisha sharti la kujisajili kwenye Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) huku ikiwa hajapewa muda maalumu wa kukamilisha sharti hili.

"Sisi kama wizara tumepokea maombi ya Msanii Roma na niseme Mimi kama Waziri na kwa niaba ya Naibu Waziri tumemfutia adhabu Roma Mkatoliki lakini siku atakapokabidhiwa Cheti cha Usajii cha BASATA ndo siku adhabu yake itakapokuwa imekwisha" Mwakyembe.

Ameongeeza "Hatumpangii iwe lini akiweza afanye leo jioni kesho, baada ya Pasaka mwakani ni yeye, lakini siku atakapopata Cheti ndipo ataweza kuendelea na kazi zake na tunamtakia kila la kheri".

Kwa upande wa msanii Roma yeye ametoa tamko kwa mamlaka inayosimamia kazi za sanaa iweze kutoa wimbo huo katika vyombo vyote vya habari akimaanisha kuwa hataweza kuufanyia tena marekebisho yoyote kama jinsi ambavyo ilitakiwa awali.

Mwanzoni mwa mwezi Machi serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
29 March

ALIYOFUNGUKA MTANZANIA ALIYEKIMBILIA FINLAND KUNUSURU UHAI WAKE

Ansbert Ngurumo akiwa Finland

Mwandishi wa habari mwandamizi Ansbert Ngurumo ambaye amekimbilia ulaya nchini Finland kwa kile anachokiita kuwa ni kunusuru maisha yake, amezungumza na BBC.

Ngurumo ambaye amefanya kazi na vyombo kadhaa vya habari nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na gazeti la Mwanahalisi ambalo limefungiwa hivi karibuni, anaishutumu serikali kwa kupanga njama hizo za kutoa uhai wake.

Lakini Msemaji wa serikali amepuuza madai hayo ya Bwana Ngurumo na kusema Ngurumo amekimbia kwa sababu zake binafsi na kwamba uhuru wa habari na kujieleza nchini Tanzania ni wa uhakika.

Aliyefanya mahojiano na wote hawa ni mwandishi wa BBC, Sammy Awami na haya ndio mazungumzo yao:

Sammy: Hii ni mara ya kwanza kwa mwandishi wa habari wa Tanzania, kukimbia nchi yake na kudai kuomba hifadhi katika nchi nyingine kwa madai ya kuwa hatarini kutokana na kazi yake ya uandishi wa habari.

Ngurumo: Kimsingi yaliyonikuta ni marefu sana lakini la msingi ni kuwa nimekimbia, nimejificha najihadhari na ni tofauti na wanaosema nimeikimbia nchi, mimi sijaikimbia nchi, nchi ni ya kwangu, mimi ni mtanzania na najua mambo haya yataisha na nitarudi. Lakini kitu kikubwa ni kwamba nimewakimbia wauwaji, nimekimbia watesaji , nimekimbia watu wanaowateka watu ambao wanalindwa na dola..

Sammy:Umetoa shutuma kwamba hawa watekaji, wanaoua watu, wanalindwa na dola, hizi ni shutuma nzito sana Bwana Ngurumo, una uthibitisho gani kuwa dola inawalinda hawa watu?
Ansbert Ngurumo alikuwa akiandikia gazeti la MwanaHalisi

Ngurumo: Kama hutaki kuituhumu dola katika mazingira haya, unamtuhumu nani ambaye anapaswa kushughulikia haya? Amepotezwa Azory mwandishi habari wa Mwananchi, waajiri wake na wafanyakazi wenzake wameandamana wametaka arudi. Leo ni zaidi ya siku 100 hajulikani alipo, serikali iliyohai inayofanya kazi, inayolinda uhuru wa raia, haitoi majibu nani atuhumiwe kama si wao?

Sammy: Lakini serikali inasema inaendelea na uchunguzi wa matukio yote haya,kwa nini usiiamini?

Ngurumo: Vitendo na mwenendo na tabia yake vinaifanya isiaminike, kwa sababu hatuoni ikichunguza. Kama serikali inaweza kukamata watu wanaoikosoa haraka, ikawapeleka mahakamani, inashindwa nini kukamata watu wanaowaua wanaoikosoa.

"Ninaandika kwenye ukurasa wangu kwa mara ya kwanza baada ya miezi minne tangu Oktoba 2017. Ninamshukuru Mungu na Wasamaria wema kwa kunisaidia na kuiokoa maisha yangu kutoka kwa mikono ya 'watu wasiojulikana' Tanzania

Sammy: Wewe ulifanya nini, ulisema nini, uliandika nini hata hawa unaowashutumu kutaka kukutoa uhai kukufuata?

Ngurumo: Nimekuwa naandika kwenye magazeti kwa zaidi ya miaka 20 lakini kwa miaka kama 15, nimekuwa na makala ya maswali magumu imekuwa inawauma sana na kuwakera watawala. Utawala uliopita ulikuwa pamoja na kuchukia, ulikuwa unavumilia na wakati mwingine kufanyia kazi, lakini utawala ulioingia umekuwa hautaki kuguswa wala kukosolewa.

Sammy: Lakini Bwana Ngurumo, haya unayoyasema wewe si mwandishi pekee ambaye umekosoa serikali,kuna waandishi wengi na hata viongozi wa dini na watu wengine wamekuwa wakikosoa vitendo hivi kwa nini wakufuate wewe tu?

Ngurumo: Hilo swali waulize wao lakini wameshapotea wengi kabla yangu , tofauti yangu na wengine ni kuwa mimi ni mepata bahati tu ya kutonywa.

Serikali yasemaje kuhusu shutma hizo?

Serikali ya Tanzania nayo imekanusha madai hayo, mwandishi wetu Sammy alizungumza na Dk. Hassan Abbas ambaye ni msemaji wa serikali ya Tanzania. Haya hapa ni mazungumzo yao:

Sammy :Bwana Ngurumo anaishutumu serikali kutaka kutoa uhai wake kwa sababu ya kazi yake unalizungumziaje
Dk Hassan Abbas

Dk.Abbas: Mimi niseme kuwa madai yake hayana msingi na labda ana ajenda zake ambazo nafikiri tusubiri kuziona kwa sababu serikali ya Tanzania imesajili vyombo vingi vya habari na ndio inayoruhusu mwanahabari kufanya kazi zake na kila mwanahabari anatekeleza kazi zake kwa misingi ya taaluma

Sammy: Anatoa mifano ya watu wamepotea, kwa sababu za kisiasa, anaamini kuwa kuna watu wanakamatwa, na yeye kwa kuwa amekuwa akikosoa serikali kwa muda mrefu ndio sababu anadai serikali inataka kutoa uhai wake?

Dk.Abbas: Mimi nafikiri Ngurumo tumsaidie, watu wanaodai kuwa mtu fulani amechukuliwa hatua kwa sababu ya kazi yake au kukosoa, nafikiri hawaitendei haki nchi, hakuna sheria ya nchi hii inayounda kosa la kukosoa serikali.
Visa vya mauaji ya kutoweka kwa watu Tanzania
Mauaji ya Kibiti mwaka 2017: Viongozi wa CCM, askari zaidi ya 10 na wananchi karibu 40 katika eneo la Kibiti walishambuliwa na kuuawa na watu wasiojulikana.
11 Februari, 2018 Kiongozi wa Chadema Daniel John alitekwa na kisha aliuwawa kikatili wakati wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni. Mwili wake ulipatikana mnamo 14 Februari.
Mnamo 7 Septemba, 2017, Mnadhimu Mkuu wa upinzani bungeni, mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Area D Mkoani Dodoma. Bw Lissu pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.
21 Novemba, 2017 Mwandishi wa habari wa Mwananchi Communications Limited Azory Gwanda alipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka sasa hajapatikana.
Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Ben Saanane alipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Sammy:Kwa hiyo unahakikishia watu kuwa uhuru wa kujieleza na habari tanzania uko safi kabisa?

Dk.Abbas:Uko salama kwa mujibu wa vigezo vya kisheria, kwamba waandishi wa habari wanafanya kazi yao kwa hiyo nafikiri Tanzania tuko salama tunaendelea vizuri, niwaambie wana habari watimize wajibu wao wasitengenezewe hofu isiyokuwepo lakini kikubwa tunazo sheria na taratibu za taaluma yetu.

Kuhusisha suala la Azory kutekwa au kupotea na serikali; tujiulize suala moja, Azory ameandika kitu gani cha kukosoa kikaiudhi serikali?

Maendeleo makubwa ambayo tunafanya kwenye nchi yetu hayawezi kuwapendeza wengi kwa hiyo tunajua wako watu watapika mambo mengi kisiasa lakini sisi tunasimama kuzingatia misingi ya sheria za nchi .

Tukitoa mfano wa Sugu, alisimama mahakamani akajitetea akachukuliwa hatua, ukitoa mfano wa Azory aliandika nini na wapi dhidi ya serikali mpaka kukawa na kiashiria kama hicho? mimi nafikiri tunahusisha matukio fulani ambayo hayana uhusiano na serikali.

Sammy: hili suala la uhuru wa kutoa habari, kupokea na kujieleza limezungumzwa na makundi mengi, asasi za kiraia,jumuia ya kimataifa na hivi karibuni waraka wa maaskofu imeelezwa kumekuwa na uminyaji uhuru wa kujieleza kutoa maoni yao kwa ujumla , wanauliza kwa nini Tanzania imefikia hatua hii?

Dk.Abbas:Mjadala wa uhuru wa kujieleza uko sehemu zote duniani ,mjadala kuhusu weledi wa waandishi wa habari na usahihi wa habari zinazotolewa, unaposema haki ya kupata habari si habari zozote, bali habari sahihi, na kuna misingi ya kufuata. misingi yakitaaluma isipofuatwa kuna hatua za kisheria zitachukuliwa.Ukimdhalilisha mtu ukichukuliwa hatua huwezi kusema ni kukiuka uhuru wa habari .Ukiingilia usalama wa taifa nchi zote duniani zinalinda usalama wake ukiingilia unachukuliwa hatua.

Chanzo: BBC 📻
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Sunday, 25 March 2018

25 March

ASKOFU DR MUNGA ATOA SOMO KUNTU KWA VIONGOZI

Askofu Stephen Munga kushoto akisalimia na rais mstaafu Jakaya Kikwete
Anazungumuza haya Dr Munga

KUTENGENEZA HISTORIA YAKO NZURI YA KUDUMU

"Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu."
(Matayo 5:8).

Hili ni fundisho lingine zito la Yesu Kristo ambalo mara nyingine tumelichukulia juujuu. Tuanze na swali: moyo safi ni moyo wa namna gani? Moyo safi ni moyo uliotakasika ambao ndani yake hakuna hila wala unafiki. Katika "posting" yangu hapa niliwahi kuzungumzia juu ya unafiki na jinsi Yesu Kristo alivyojitenga nao na kupambana na unafiki na wanafiki. Pale nilisema kwamba hata hukumu yake ya kifo ni matokeo ya mapambano hayo. Moyo safi ni moyo uliojazwa upendo, kweli na haki. Hao waliojazwa hayo mioyoni mwao wanapewa na zawadi ya kuwa waaminifu kwa dhamiri zao katika kutetea tunu (virtues and values) hizo. Kwa hiyo wenye moyo safi ni watu ambao wanazo dhamiri safi katika kutetea upendo, kweli na haki katika maisha yao. Hao ndio watu wale ambao wanaahidiwa kumuona Mungu. Lakini je, kumuona Mungu kunamaanisha nini katika maisha yetu?

Kumuona Mungu maana yake ni kwamba kumbukumbu za watu wa jinsi hiyo zinavuka mipaka ya maisha haya. Mungu ndiye ukamilifu na utimilifu wa historia zetu. Mungu ni wa milele. Mungu anavuka mipaka ya historia ya ulimwengu tunamoishi. Kwa hiyo historia ya watu wenye moyo safi ni historia inayovuka mipaka ya maisha haya tunayoishi ulimwenguni humu. Wapo watu waliotaka kuwa mashujaa mfano wa Hitler na Idi Amin wa Uganda lakini kwa sababu hawakuwa na mioyo safi, basi historia imewatema. Hatuwakumbuki watu wa jinsi hiyo kwa mema bali tunawakumbuka kwa jinsi walivyojaribu kuubomoa ulimwengu na jamii zake. Watu wa jinsi hiyo ni wale ambao wanajitafutia utukufu wao binafsi. Kwa kuwa historia haifungwi bali ni mtiririko wa maisha kuelekea umilele, basi historia za watu wa jinsi hiyo hukatika. Historia haitakuja itokee itunze watu wa jinsi hiyo kama waliokuwa na nia ya kuujenga ulimwengu kwa mema. Walijitahidi kitumia mkono wa chuma kuumiza na kuangamiza watu na jamii zao lakini hatimaye historia iliwageuka na kuwaanika kama wasaliti wa jamii za ulimwengu.

Wakati mwingine tunapopata madaraka na mamlaka tunageuka na kujifanya miungu ya dunia. Tuanataka kila mtu atutii sisi na kuiacha njia ya kumtii Mungu wa kweli. Lakini tunafanya hayo kwa kujisahau kwamba hata sisi maisha yetu ni ya muda tu. Kila mmoja wetu anapewa nafasi ya kutengeneza historia yake chini ya mbingu. Fursa hii ya uhuru anaotupa Mungu mara nyingi tumeitumia vibaya. Tunasahau kwamba historia yetu inayodumu ni ile ambayo imesimama katika kuwa na mioyo safi iliyojengeka katika upendo, kweli na haki na kuyatunza hayo kwa dhamiri safi. Mfalme Daudi na watawala wote waliofanikiwa walitambua hivyo. Tusingekuwa tunaziimba Zaburi za Mfalme Daudi kama asingefanya hivyo. Tusingemuita Nyerere kuwa Baba wa Taifa kama asingetambua na kufanya hivyo. Hawa na wengine tunaowatambua tumeendelea kuwaheshimu ng'ambo ya vifo vyao kwa sababu walikubali kuvikwa mioyo safi. Historia zao zinabaki kwetu kwa sababu walitunza tunu za upendo, kweli na haki. Kwa maisha yao na dhamiri zao safi wamefanya mambo ambayo yalilenga katika kuhifadhi ulimwengu na jamii zake.

Mwisho niseme kwamba watawala wengi wamekuwa chambo cha dhamiri mbovu za maangamizi. Historia haijawahi kuhifadhi kumbukumbu njema kwa watu wenye roho chafu na mbaya. Kama ambavyo historia haikuwahifadhi watu wa jinsi hii ni wazi kwamba hawakufikia upeo wa juu wa historia -yaani kumuona Mungu (labda pale walipotubu) lakini hayo ni mambo ya siri ambayo hatuyatambui na kuyaweka katika historia bali tunamwachia Mungu mwenyewe. Kwa jinsi hiyo basi ili historia ikutambue na kukuweka katika historia inayovuka ng'ambo ya maisha haya ni vema kujitaabisha katika kutunza dhamiri yako inayojengwa katika upendo, kweli na haki. Hii inadai mabadiliko makubwa ya ndani. Kinyume cha hapo lazima historia itakutema hata kama unajigamba kwa majivuno makubwa. Mungu ni utimilifu wa historia za watu wote wenye mioyo safi. Tena Mungu ndiye anayeupatia ulimwengu hekima ya kufuta historia ya watu wote waletao maangamizi kwa kujifanya wao ni miungu ya ulimwengu huu.

USIJIDANGANYE. WEWE SI KITU PALE UNAPOFUATA MOYO WAKO MCHAFU!!! Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Saturday, 24 March 2018

24 March

ZITTO AMEAMUA KUTEMA CHECHE, ADAI YUPO TIARI KWA KIFO

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe


Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa yupo tayari kusema asante siku yake ya kutwaliwa ikifika kwani anauhakika amejitahidi sana katika kuuweka mkoa wake wa Kigoma kwenye ramani.

Zitto ameyasema hayo kupitia waraka wake ambapo amedai kwamba Kiongozi huwa anawaza kizazi kijacho na mwanasiasa huwaza uchaguzi ujao na kwa upande wake wakati anaingia bungeni alimuomba Mungu amsaidie kupitia yeye watu waone ufakhari kutoka Kigoma.

Aidha Zitto ameongeza kwamba hakuna mtu wa Kigoma anayeoona aibu kusema anatoka Kigoma hiyo ni kutokana na mshikamano walioutengeneza.

"Leo hata mola akisema Bwana Mwami funga siku zimetimia, nitasema Asante Mungu. Nitakuwa natabasamu maana nimeweka tofari zangu kupandisha nyumba yetu Kigoma juu ya msingi Imara kabisa. Watoto na Wajukuu watasema alikuwepo Mwami. Alikuwepo Kiongozi. Wataendeleza kazi" Zitto.

Ameongeza kwamba wanaowaza "Uchaguzi unaofuata hawana miadi na mungu. Wanaojiapiza kuhusu uchaguzi unaokuja hawajawahi hata kuchaguliwa kwenye kitongoji cha kwao walipozaliwa".

Mbali na hayo Mbunge huyo amefunguka kwamba demokrasia ndiyo imetoa nguvu kubwa ya kupiga hatua ikiwa ni pamoja na sauti ya kusikika "Anayetaka turudi kwenye ukiritimba ni adui mkubwa. Tutampiga tu".
 
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Thursday, 22 March 2018

22 March

WARAKA WA MBOWE WAIBUA MAZITO


Viongozi Waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Leo Machi 22, 2018, viongozi Waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wametakiwa kuripoti tena katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam ambapo kwa muda wa wiki tano sasa wametakiwa kuripoti kituoni hapo kila wiki tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa majimbo ya Kinondoni na Siha.
Mbowe amesema kuna njama za kuwahusisha na tuhuma mbalimbali.EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
22 March

MPANGO WA TRUMP WA VIKWAZO ZIDI YA CHINA WAZUA HOFU


.
Rais Xi-Jinping wa China na mwenzake Donald Trump wa marekani

Utawala wa rais Trump unapanga kutangaza vikwazo dhidi ya China siku ya Alhamisi baada ya kubaini kwamba taifa hilo linashinikiza wizi na uhamisho wa ubunifu kutoka biashara za Marekani.

Ikulu ya whitehouse imesema kuwa hatua hiyo inajiri baada ya miaka kadhaa ya mazungumzo yalioshindwa kupata suluhu kuhusu wala hilo.

Vikwazo hivyo vitashirikisha ushuru na masharti mengine.

Mpango huo umezua hofu kuhusu vita vya kibiashara. Ikulu ya whitehouse iliripotiwa na vyombo vya habari vya Marekani kuweikea ushuru wa kati ya $30bn-$60bn kwa mwaka pamoja na masharti ambayo yatazuia uwekezaji .

Vilevile huenda Marekani ikawasilisha malalamishi yake kwa shirika la biashara duniani WTO, kulingana na maafisa wa biashara.

Mpatanishi mkuu wa biashara nchini Marekani Robert Lighthizer aliambia wabunge wa Congress siku ya Jumatano kwamba Marekani inafaa kuiwekea China shinikizo kali na shinikizo ya chini watumiaji wa Marekani.

Bwana Lighthizer amesema kuwa kulinda ubunifu ni muhimu kwa uchumi wa Marekani.

''Ni swala mushimu sana'' , alisema bwana Lighthizer. ''Nadhani kitakuwa kitu muhimu ambacho kitafanyika katika kuleta usawa wa kibiashara''.

Je nini kilichoshinikiza kuwekwa kwa ushuru huo?

Afisa wa biashara nchini Marekani ambaye alizungumza na wanahabari alisema kuwa Marekani ina ushahidi kwamba China inataka kampuni za Marekani kuingia katika ushirikiano na kampuni za China ili kuingia katika soko la taifa hilo kwa lengo la kuzishinikiza kampuni hizo kuhamisha teknolojia yao
Marekani pia iligundua kwamba China inawekeza katika kampuni muhimu za Marekani na kufanya mashambulio ya mitandao.

Matokeo hayo yanatoka katika uchunguzi ulioagizwa na rais Trump mwezi Agosti kwa jina 301.

Katika kipengee cha 301 cha sheria ya biashara, serikali imejipatia uwezo wa kuwekea vikwazo mataifa ambayo inahisi hayafanyi biashara kwa usawa.

Bwana Trump mara kwa mara amekuwa akilalamika kuhusu ukosefu wa usawa kibiashara kati ya Marekani na China.
Je hatua hiyo inaungwa mkono na wengi?

Kuna wasiwasi mkubwa nchini Marekani kwamba China inatafuta teknolojia ambayo wanaweza kuitumia kijeshi. Bunge la Congress pia linapanga kupitisha sheria ambayo itaipatia serikali uwezo wa kubadilisha mikataba ya biashara za kigeni kutokana na vitisho vya kununua viwanda vya Marekani.

Lakini wanasiasa na viwanda ikiwemo watumiaji wameonyesha wasiwasi kwamba huenda China ikalipiza kisasi.

Bwana Lighthizer amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa China ikalipiza kisasi akidai kwamba Kilimo cha Marekani huenda kikaathiriwa , lakini akasisitiza kwamba hatua hiyo haitaizuia Marekani kuchukua hatua.

Iwapo watalipiza kisasi basi Marekani italazimika kuwalinda wakulima wake.

Je China imesema nini?

China imesema kuwa hakutakuwa na mshindi yeyote katika vita vva kibiashara.

Siku ya Jumanne , siku ya mwisho ya kikao cha kila mwaka cha chama tawala cha taifa hilo, kiongozi wa China Le Keqiang amesema kuwa ombi lake ni kwamba pande zote mbili zinafaa kutulia.

Pia alisema kuwa anatumai kwamba Marekani itapunguza masharti kuhusu bidhaa za kiteknolojia zinazoingia China.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Wednesday, 21 March 2018

21 March

MWAKYEMBE AFUNGUKA MAZITO BIFU LA MONDI NA SHONZAWaziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa amesikitishwa na matamshi ya msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakati akihojiwa na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommy, kwa hatua ambazo Wizara inachukua kulinda maadili ya Kitanzania katika tasnia ya sanaa.

Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo na wasanii wawili kwa kukiuka maadili, yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza anayemlaumu. Diamond atambue kuwa Serikali ina taratibu zake. Maamuzi ya Naibu Waziri ni maamuzi ya Wizara.Kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, however popular he is. Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake.Si busara kwake kushindana na Serikali, na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya. Sijafurahishwa hata kidogo.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ