BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts

Thursday, 7 June 2018

07 June

VIWANGO VIPYA VYA FIFA LEO JUNE 7


Wakati tumebakiza siku 8 kuelekea kombe la dunia litakalofanyika nchini urusi leo fifa wametoa viwango vipya vya ubora duniani kwa timu za taifa kwa upande wa wanaume.

England hawapo kwenye top 10 ya orodha hiyo licha ya kufanya vizuri kwenye mechi 10 zao za mwisho.

Orodha kamili

1.Ujerumani
2.Brazil
3.Ubelgiji
4.Ureno
5.Agentina
6.Switzerland
8.France
9.poland
10. Hispania
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
07 June

"KWAHERI DEUS KASEKE"


  Mchezaji nyota wa singida united deus kaseke anaweza asiwe katika kikosi cha singida united msimu ujao.

  Taarifa toka klabu ya singida united kupitia mkurugenzi wake festo sanga zinasema kwamba deus kaseke hatakuwa katika kikosi hicho msimu ujao.

  Taarifa hizo zimekuja baada ya Deus kaseke kutakiwa na klabu inayoshiriki ligi kuu Afrika kusini. lakini klabu hiyo haikutajwa mpaka usajili wake utakapokamilika.EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
07 June

SOMA ALIVYOFUNGUKA MSUVA KUHUSU KICHUYA

Kiungo mshambuliaji Mtanzania anayekipiga Klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva, amepata taarifa za kiungo wa Simba, Shiza Kichuya kuwaniwa na TP Mazembe ya DR Congo na kumwambia ndiyo wakati huu aondoke Msimbazi.

Kauli hiyo, ameitoa hivi karibuni baada ya kupata taarifa za kiungo mkabaji wa Azam FC, Himid Mao, kutua Klabu ya Petrojet ya nchini Misri akiwa kama mchezaji huru.

Wakati Msuva akimpa mchongo huo Kichuya, tayari Kichuya ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Akizungumza na Global Tv Online, Msuva alisema anafurahia kuona idadi ya wachezaji wa hapa nchini wakipata ofa za kwenda kucheza nje ya nchi kama ilivyokuwa kwake, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa na Himid.

Msuva alisema, anaamini Kichuya ana uwezo wa kucheza nje ya nchi ikiwemo Congo kwenye timu ya Mazembe ambayo imeonyesha nia ya kumsajili, hivyo ni wakati wake wa kutoka nje ya nchi kwenda kutafuta changamoto mpya.

“Nimepata taarifa za Kichuya kuhitajika Mazembe kwa ajili ya kwenda kucheza soka la kulipwa, niseme ni nafasi nzuri kwake kwenda kutafuta chagamoto nyingine mpya nje ya nchi.

“Ninafurahia kuona idadi ya wachezaji ikiongezeka ya kwenda kucheza soka la kulipwa, hiyo itatusaidia sisi kuitangaza nchi na kuwavutia mawakala na kuja kuchukua wachezaji wengine.”

“Nimefurahia kuondoka kwa Himid hapa nchini na kwenda kujaribu changamoto Misri yenye ligi ya ushindani, hivyo kutasaidia kutengeneza timu bora ya taifa.

Simon Msuva

Wednesday, 6 June 2018

06 June

ORODHA MPYA YA WANAMICHEZO MATAJIRI DUNIANI


Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika porodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.

Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi yake ya masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani.

Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhfa wa pili kwa tofauti ndogo.

La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake katika orodha hiyo baada ya mwanamke wa pekee katika orodha hiyo Serena Williams kutoorodheshwa.

Wachezaji 100 bora walijipatia jumla ya $3.8bn, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 23 kutoka mwaka uliopita ,Forbes ilisema

Dereva wa magari ya F1 Lewis Hamilton ndio mwanamichezo Muingereza anayelipwa kipato cha juu cha $51m akiwa nambari 12.

Mayweather ambaye jina lake la utani ni Money-aliongeza kipato chake cha michezo kwa $10m

"Mechi kubwa kati yake na McGregor 2017 iliwasaidia Mayweather na McGregor kujipatia pato la jumla ya $400m'' , alisema Kurt Badenhausen, Mhariri mkuu wa jarida wa Forbes Media.

"Lakini wachezaji wa mpira wa vikapu wametawala orodha ya wanamichezo 100 kufuatia kuongezwa kwa mishahara yao inayotokana na kandarasi ya maouyesho ya runinga ya $24bn

Aliongezea: "Orodha ya Forbes' ya wachezaji wanaopata mapato ya juu imejaa wanaume. lakini kumekuwa na mchezaji mmoja wa kike ambaye alifuzu baada ya orodha hiyo kuongezwa hadi majina 50 2010.


Wanamichezo 10 tajiri zaidi duniani.


  1. Floyd Mayweather - Ndondi ($285m)
  2. Lionel Messi - Kandanda ($111m)
  3. Cristiano Ronaldo -Kandanda($108m)
  4. Conor McGregor - Karate, judo na Ndondi ($99m)
  5. Neymar - kandanda ($90m)
  6. LeBron James - Kikapu ($85,5m)
  7. Roger Federer - Tenisi ($77.2m)
  8. Stephen Curry - Kikapu ($76.9m)
  9. Matt Ryan - Soka ya Marekani ($67.3m)
  10. Matthew Stafford - Soka ya Marekani ($59.5m)
06 June

KWA VIGINGI HIVI KAKAMEGA AJIPANGE!


Kakamega homeboys


Na mwandishi wetu Edusportstz habari

Kesho tarehe 7june kutakuwa na mtanange wa kukatana shoka kati ya Simba sports club toka Tanzania  na kakamega homeboys toka nchini Kenya. Hata hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana mambo yafuatayo

Simba atataka kuionesha kakamega homeboys kuwa  wao ni wapinzani wakweli na homeboys walimbahatisha tu yanga kwakuwa yanga ni kibonde wao. Lakini pia Simba atataka kumuonyesha kwamba ana uwezo wakubeba makombe ndani na nje ya Tanzania.Lakini pia Simba itatka kumuonyesha Yanga kuwa wao wanao uwezo wakumpiga Yanga akiwa nyumbani na kumpiga mbaka mbabe wake (kakamega homeboys) yaani hawabahatishi.

Ugumu mwingine ni kwamba Homeboys hatakuwa tayar kuachia kombe lije Tanzania atajitahidi kutumia kila mbinu ili walibakize timu nchini kwao Kenya.Lakini pia Kakamega Homeboys watataka kuutumia  uzoefu walionao katika viwanja vya nyumbani kwao yaani Kenya

SWALI KWAKO MSOMAJI WAKO NANI ATAINGIA FAINALI SIMBA KAKAMEGA HOMEBOYS?

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Tuesday, 5 June 2018

Monday, 4 June 2018

04 June

VIONGOZI YANGA WAISUSIA TIMU


Hali imezidi kuwa mbaya kwenye klabu ya yanga baada ya kumaliza msimu nafasi ya 3 huku wakiwa na matokeo mabaya toka kocha wake mkuu george lwandamina alipoiacha timu hiyo.

kuondoka kwa george lwandamina kulielezwa kwamba ni mipango mibovu ndani ya klabu hiyo.

Lakini hali imezidi kuwa mbaya zaidi baada ya kiongozi mwingine kuachia nafasi hiyo.

Mkemi ni moja ya kiongozi wa yanga alieachia nafasi yake rasmi ndani ya klabu hiyo baada ya kile alichokisema kupitia ukurasa wake wa instagram, kupisha mawazo na misingi mipya ndani ya klabu hiyo ili kuikoa ilipo.

mkemi aliyehudumu ndani ya klabu hiyo kwa mafanikio makubwa sana. Ameng'atuka rasmi na atabaki kama mwanachama tu wa klabu hiyo.


Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ