PHIRI Mchezaji Bora Simba SC September 2022 - EDUSPORTSTZ

Latest

PHIRI Mchezaji Bora Simba SC September 2022

PHIRI Mchezaji Bora Simba SC September 2022

PHIRI Mchezaji Bora Simba SC September 2022

PHIRI Mchezaji Bora Simba SC September 2022

PHIRI MCHEZAJI BORA SIMBA

Mshambualiaji kinara wa Klabu ya Simba SC, Moses Phiri amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompa hadi kufanikiwa kuibuka mshindi katika Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi September (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Phiri amesema kuwa Ushirikiano aliopata kutoka kwa wenzake ni mkubwa ba anaamini ataendelea kufunga na kuchukua tuzo hiyo mara kwa mara kutokana na kuzungukwa na wachezaji bora.

Phiri ameibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kuwazidi nyota wenzake wawili Clatous Chama na Mzamiru Yassin alioingia nao Fainali.

“Nawashukuru wachezaji wenzagu kwa kunipokea na kunipa ushirikano ndani na nje ya pia nawashukuru mashabiki kwa sapoti yao na kunipigia kura zilizoniwezesha kupata tuzo hii.Tuzo hii inatuhamasisha sisi wachezaji kufanya vizuri na kuipigania timu.

“Naamini nikiendelea kupata sapoti kutoka kwa wachezaji wenzangu naweza kuchukua tuzo hii hata kila mwezi,” amesema Phiri.

Katika mwezi September Phiri amecheza mechi nne akifunga mabao matatu na kusaidia mengine mawili (assist) baada ya kucheza dakika 334.

Kwa kushinda tuzo hiyo Phiri amekabidhiwa pesa taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

The post PHIRI Mchezaji Bora Simba SC September 2022 appeared first on Nijuze Mpya.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz