Wema Sepetu Ataja SIFA Kadhaa za Mwanaume Anayempenda...Kama we ni Mfupi na Wanuka Kwapa Sahau - EDUSPORTSTZ

Latest

Wema Sepetu Ataja SIFA Kadhaa za Mwanaume Anayempenda...Kama we ni Mfupi na Wanuka Kwapa Sahau


Katika mapenzi kila mtu ana kigezo cha kumpata mpenzi anayempenda. Supastaa Wema Sepetu ametaja sifa za mwanaume anaempenda na kusema kuwa anapenda mwanaume wake awe mrefu kuliko yeye na awe hanuki kwapa.

Wema amebainisha hayo akiongea na mtangazaji na mshereheshaji wa shughuli mbalimbali @drkumbuka_majaliwa wakiwa safarini wakielekea visiwani Zanzibar kwenye Uzinduzi wa filamu ya Royal Tour utakaofanyika kesho Jumamosi, Mei 7. Dr Kumbuka alimuuliza Wema iwapo angepewa nafasi ya kuchagua mwanaume anayempenda angechagua mwanaume gani.

"Mwanaume wangu kwanza awe ana muonekano, mchamungu, awe mrefu kuliko mimi kwasababu mimi mrefu sana sipendi nikiwa na mwanaume nianze kuangaika kujifupisha" amejibu Wema kwa madaha.

"Awe na mapenzi ya dhati, anajua kujali na awe hanuki kikwapa (sipendi harufu mbaya)" aliongeza Wema huku Kumbuka akikazia kuwa mwanaume anenuka jasho la ndimu hatakiwi.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz