Mwanamuziki Jay Melody Afunguka Kupata Milioni 30 Kutokana na Wimbo wa Sugar - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanamuziki Jay Melody Afunguka Kupata Milioni 30 Kutokana na Wimbo wa Sugar


Mwimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya msanii @realjaymelody amefunguka kupata moja ya mafanikio ambayo hakuwahi kuyadhania awali ni kutengeneza pesa katika mitandao ya kijamii kupitia sanaa yake ya muziki.

Nyota huyo ameweka wazi kuingiza kiasi cha zaidi ya Milioni 30 za Kitanzania kupitia wimbo wake "Sugar". Ni katika shows pamoja na majukwaa mbalimbali ya kidijitali ya kusikiliza muziki mtandaoni (Digital Platforms) kwa siku chache za hivi karibuni.

"Yani 'Sugar' kiuhalisia kabisa kwa hizi siku chache chache hapa nimeingiza karibia Milioni 30, inaweza ikawa hela ndogo sana lakini mimi kwangu ni kubwa sijawahi kufanya kitu kama hicho, na nyingine bado sijatoa.'' - amesema @realjaymelody akikiambia kipindi cha The Switch cha Wasafi Fm.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz