Kundi la Mziki la Destiny's Child Kurudi Upya, Beyonce Ndani - EDUSPORTSTZ

Latest

Kundi la Mziki la Destiny's Child Kurudi Upya, Beyonce Ndani


Muimbaji wa Destiny's Child, Kelly Rowland hatimaye amenyoosha maelezo kufuatia uvumi kwamba kundi hilo (Destiny's Child) lipo mbioni kuerejea kwaajili ya kufanya muziki mpya na tamasha lao la muziki.

Kupitia mahojiano na Entertainment Tonight, Kelly Rowland amesema "Tunampenda kila mtu sana ila nadhani jambo hili linastahili kuwa la kushtukiza zaidi, kila kitu kitapangwa ila mtashtukizwa tu, itakuwa surprise mzuri".

Kundi hilo linaloundwa na mastaa watatu akiwemo Beyonce, Kelly Rowland na Michelle Williams ambao waliachana mwaka 2006 na kila mtu kufanya kazi peke yake. Ni ndoto ya muda mrefu kwa mashabiki wa kundi hilo kuona lina rejea.

Wimbo wao wa 'Survivor' ulitingisha sana na kuwapa heshima kubwa.

✍️: @omaryramsey

#SNSEnt




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz