Simba Queens Waikataa Dabi Yao na Yanga Princess bora Fountain Princess au JKT Queens-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Queens Waikataa Dabi Yao na Yanga Princess bora Fountain Princess au JKT Queens-Michezoni leo

MENEJA wa Simba Queens, Seleman Makanya, amesema kwa sasa hawana tena dabi na Yanga Princess, ni bora wahamie kwa Fountain Gate Princess au JKT Queens.

 

Makanya amekuja na kauli hiyo akiwa na maana kuwa Yanga Princess wameshakuwa wa kawaida, hiyo ni baada ya juzi Ijumaa kufungwa nyumbani na Fountain Gate Princess mabao 2-3 katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL).

 

Makanya alianza kwa kuwapongeza Fountain, kisha akatoa ya moyoni kuhusu dabi hiyo: “Hongereni sana Fountain Gate Princess kwa ushindi wa leo (juzi) dhidi ya Yanga Princess, ilikuwa mechi nzuri na yenye ushindani mkubwa.

 

“Sasa imefikia mahali tujitafakari kuangalia dabi, sasa rasmi ihamie ama kwa Fountain Gate au JKT Queens, kuanzia leo hatuna tena dabi na Yanga.”

 

Yanga Princess na Simba Queens zinatarajiwa kukutana Aprili 23, mwaka huu kwenye mchezo wao wa raundi ya pili ya ligi hiyo.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba Queens ilishinda 4-1.

SHEIKH KISHK AMVUNJA MBAVU RAIS MWINYI – ”YANGA MSITUELEWE VIBAYA”..

The post Simba Queens Waikataa Dabi Yao na Yanga Princess bora Fountain Princess au JKT Queens appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz