Chama Atangazwa Mchezaji Bora wa Mwezi Machi Awabwaga Mayele na Kahola-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Chama Atangazwa Mchezaji Bora wa Mwezi Machi Awabwaga Mayele na Kahola-Michezoni leo

 

Kiungo wa klabu ya Simba Sc, Clatous Chota Chama ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi katika NBC Premier league 2021/22 na kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya Simba kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa msimu huu wa ligi.

Chama anakuwa mchezaji wa saba kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika ligi kuu huku kwa mwezi March akiwabwaga nyota wawili Fiston Mayele (Yanga) na Frank Kahola (Mtibwa Sugar ) waliongia kwenye kinyang’anyiro cha mwezi huo.

 

Upande wa tuzo ya kocha bora wa mwezi march imekwenda kwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Sc Pablo Franco ambaye ni mara ya kwanza na yeye kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi March wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC Premier league) 2021/22 baada ya kuwa na matokeo bora kwa mwezi huo .

 

Pablo aliiongoza Simba kupata matokeo ya ushindi kwenye michezo miwili dhidi ya Biashara Mara United na dhidi ya Dodoma Jiji huku akiwashinda makocha wawili Nasreddine Nabi (Yanga Sc) na Francis Baraza ( Kagera Sugar) walioingia kwenye fainali ya mwezi March ihali tuzo ya meneja bora wa uwanja imekwenda kwa meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa ,Nsajigwa Gordon kwa kufanya vizuri kwenye michezo iliyofanyika kwenye uwanja huo kwa mwezi march na kulinda miundombinu ya uwanja kwa ujumla.

The post Chama Atangazwa Mchezaji Bora wa Mwezi Machi Awabwaga Mayele na Kahola appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz